Jun 28, 2025

WAKILI KIDYALLA ATAJA SABABU ZA KUCHUKUA FOMU ZA UBUNGE DODOMA MJINI

 WAKILI Eric Kidyalla ni moja ya makada waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania kugombea nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Jimbo la Dodoma Mjini.


Alisema sababu iliyomsukuma kuchukua fomu hiyo ni kwa kuwa yeye ni kada wa Chama hicho hivyo aliona ni vyema kutumia haki yake ya kikatiba ili akifanikiwa aweze kutoa mchango wake katika kukitumikia Chama na wanaDodoma mjini akishirikiana na watendaji wengine.

Pia amepongeza Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Jimbo la Dodoma mjini liweze kugawanyika jambo ambalo limetoa fursa kubwa kwa wanaCCM wengi kujitokeza kugombea.

"Jimbo la Dodoma mjini kijiografia lilikuwa kubwa hivyo kuridhiwa ligawanywe,  Rais, Samia amefanya jambo jema na itatoa fursa kubwa kwa wananchi,"alisema Kidyalla



Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma, Sophia Kibaba (kushoto) akimpatia fomu Wakili Eric Kidyalla ya kuomba kuwania ubunge Jimbo la Dodoma Mjini.



 Kidyala akionesha fomu hiyo.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MHARIRI

BLOG YA TAIFA YA CCM

0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages