LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 22, 2022

KINANA:BWAWA LA UMEME LA JULIUS NYERERE NI UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria Hatua ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere JNHPP kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaonesha Marais Wastaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson na Waziri wa Nishati Mhe. Januari Makamba  Njia ya kuchepusha Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115)   la Julius Nyerere JNHPP kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.

***********************

Na Selemani Msuya, Rufiji

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amesema ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Kinana amesema hayo leo wakati akitoa salamu za CCM kwenye hafla ya zoezi la ujazaji maji kwenye Bwawa la JNHPP iliyoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kushuhudiwa na Marais wastaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete, Spika Dk Tulia Ackson na wengine wengi.

Alisema matarajio yao ni baada ya mradi huo kukamilika utapunguza makali ya bei ya ununuzi wa umeme, lakini pia utakuwa bora na salama.

“Hiki ambacho kinafanyika leo hapa ni cha kupongezwa sana, kwani Ilani ya CCM inatekelezwa, tumpongeze Rais Samia kwa uthubutu huo,” alisema.

Kinana alisema katika kuhakikisha wanazungumzia mradi huo kwa kina wanatarajia kufanya ziara ya kichama katika mradi huo.

Alisema chama kipo pamoja na Rais Samia katika kutekeleza miradi mbalimbali nchini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages