LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 20, 2025

SONGEA WAMSUBIRI KWA HAMU DKT. SAMIA, WAAHIDI KUMPIGIA KURA

 Baadhi ya vijana wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo mama lishe, fundi mchundo, wauza viatu vya mtumba na bodaboda wa Songea mjini, Mkoa wa Ruvuma,  wakielezea kufurahishwa na utendaji mzuri  wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea maendeleo makubwa ikiwemo ujenzi wa barabara, hospitali, shule na utoaji mikopo isiyo na riba. 


Kwa mambo makubwa yaliyofanywa na Dkt. Samia Songea na Mkoa mzima wa Ruvuma, vijana hao niliofanya nao mahojiano leo Septemba 20, 2025,  wameahidi kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025. 

Dkt. Samia anatarajia kuingia Mkoa wa Ruvuma kesho Septemba 21, 2025 na kujumuika pamoja na Mgombea Mwenza ambaye ni mzawa wa mkoa huo, Dkt. Emmanuel Nchimbi katika mikutano ya kampeni mkoani humo.

Mama Lishe Shani Baraka.

Fundi Mchundo Hamis Bilali.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages