Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaahidi wakazi wa Mkoa wa Dodoma kuwa endapo chama hicho watakipatia ridhaa ya kuchaguliwa tena, kitaenda kumaliza tatizo la maji katika mkoa huo na kuwa hakutakuwa na shida ya maji.
Amesema changamoto hiyo ya maji itatatuliwa kupitia mradi mkubwa utakaoanza kutoa maji kutoka Ziwa Victoria mkoani Mwanza hadi Dodoma pamoja kukamilisha ujenzi wa bwawa kubwa la maji la Farkwa.
Aidha, amesema kuwa Serikali anayoiongoza imeimiminia Dodoma zaidi ya Sh. Tril. 9 za ujenzi wa zaidi ya miradi 3000 miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni jijini Dodoma Agosti 31, 2025.
Kabla ya mkutano huo, Dkt. Samia leo amefanya mikutano ya kampeni Chamwino, Chemba na Kondoa.



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇