LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 31, 2025

PICHA ILIYOBEBA UJUMBE MURWA KATIKA MKUTANO WA KAMPENI WA DKT. SAMIA DODOMA


 Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akionesha kikapu chenye ujumbe huo muhimu wakati wa mkutano wa Kampeni za Mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan  katika viwanja vya Tambukaleli jijini Dodoma Agosti 31, 2025.


Akielezea baadhi ya mafanikio yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita na kuleta fursa za ajira katika mkoa huo ametaja kuwa  ni; kuvutia wawekezaji kwa kujenga viwanda, Soko la Machinga, Barabara ya mzunguko, Reli ya SGR, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na  Uwanja wa mkubwa wa kisasa wa Mpira.


 Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaahidi wakazi wa Dodoma kuwa endapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuchaguliwa tena, kitaenda kumaliza tatizo la maji katika mkoa huo na kuwa hakutakuwa na shida ya maji.


Amesema changamoto hiyo ya maji itatatuliwa  kupitia mradi mkubwa utakaoanza kutoa maji kutoka Ziwa Victoria mkoani Mwanza hadi Dodoma pamoja kukamilisha ujenzi wa bwawa kubwa la maji la Farkwa.


Kabla ya mkutano huo, Dkt. Samia leo amefanya mkiutano ya kampeni  Chamwino, Chemba na Kondoa.


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages