LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 29, 2021

IGP SIRRO AITAKA NIC KUHAKIKISHA INATOA ELIMU YA KUTOSHA KWA JESHI LA POLISI KUJIUNGA NA BIMA ZA MAISHA

 

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza katika hafla ya Kuandikishina hati ya makubaliano kati ya Shirika la Bima la Taifa NIC na jeshi la polisi iliyofanyika Makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt. Elirehema Doriye  akizungumza katika hafla ya Kuandikishina hati ya makubaliano kati ya Shirika la Bima la Taifa NIC na jeshi la polisi iliyofanyika Makao makuu ya shirika hilo leo Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la TPFCS, Bw. Toi Ruvumbagu akizungumza katika hafla ya Kuandikishina hati ya makubaliano kati ya Shirika la Bima la Taifa NIC na jeshi la polisi iliyofanyika Makao makuu ya shirika hilo leo Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt. Elirehema Doriye (Kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la TPFCS, Bw. Toi Ruvumbagu wakiandikishana hati za makubaliano kati ya mashirika hayo mawili leo makao makuu ya NIC Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt. Elirehema Doriye (Kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la TPFCS, Bw. Toi Ruvumbagu wakionesha hati za makubaliano baada ya kuandikishana kati ya mashirika hayo mawili leo makao makuu ya NIC Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipata picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) katika hafla ya Kuandikishina hati ya makubaliano kati ya Shirika la Bima la Taifa NIC na jeshi la polisi iliyofanyika Makao makuu ya shirika hilo leo Jijini Dar es salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amelitaka Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuhakikisha linatoa elimu ya kutosha kwa jeshi la polisi kuhusu umuhimu wa kuwa na bima za maisha ili kuwezesha askari wengi kujiunga na huduma hiyo kwa maana wapo kwenye liski katika kazi zao.

Ameyasema hayo leo IGP Sirro katika hafla ya Kuandikishina hati ya makubaliano kati ya Shirika la Bima la Taifa NIC na jeshi la polisi iliyofanyika Makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es salaam.

IGP Sirro amesema kuna ulazima shirika la bima la NIC kutanua wigo na kuweza kuwafikia watanzania wengi waweze kupata uelewa wa huduma za bima na kuweza kujiunga na huduma hiyo kwani inamanufaa makubwa kwa watanzania.

“Vijina wetu wamekuwa wakigongwa na magari katika kazi zao za kupitisha magali barabarani, unamsimaisha deeva amelewa aangalii huyu ni askari polisi anamgonga kwahiyo kuwa na bima ya maisha ni jambo la msingi  sana”. Amesema IGP Sirro.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt. Elirehema Doriye amesema Shirika linatoa huduma zote za bima za maisha na bima za mali na ajali, kwa kutoa huduma hizo pia inafanya huduma za uwakala wa shirika la uzalishaji mali la jeshi la polisi kuwa na wigo mpana zaidi kwa kuwafikia watanzania.

“Kupitia uwakala utawezesha jeshi la polisi,maafisa,wafanyakazi pamoja na familia zao na watanzania wote kupata huduma zote za kibima kupitia wakala washirika la uzalishaji mali la jeshi la polisi”. Amesema Dkt.Doriye.

Pamoja na hayo Dkt.Doriye amesema kupitia mahusiano yao na Shirika la uzalishaji mali la jeshi la polisi watakuwa wanaenda kutekeleza mpango mkakati wa maendeleo ya sekta ya bima ambao kwa kiasi kikubwa utaongeza ufahamu wa bima lakini pia utumiaji wa huduma za bima

“Kwa sasa utimiaji wa huduma za bima ni asilimia 15% tu kwa watanzaniana ili tufike mpango wa serikali ambapo kufikia mwaka 2030 asilimia 50% ya watanzania wawe wanatumia huduma za bima lakini pia uelewa wa bima kwa tanzania ni chini yya asiliia 40% na mpango wa serikali ni kuhakikisha kwamba inapofika mwaka 2030 asilimia  80% ya watanzania wanaelimu sahihi ya bima”. Amesema

Hata hivyo amesema kuwa kupitia mahusiano hayo wanaenda kutekeleza pia mikakati ya serikali kuhakikisha kwamba kuna ukuaji kwenye sekta ya fedha.

Nae Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la TPFCS, Bw. Toi Ruvumbagu amesema kupitia makubaliano hayo jeshi litanufaika na fursa kama kupata wepesi wa kufikia huduma za bima kwa askari nchini, kumbukumbu zinaonesha kwamba idadi ya askari na maofisa wa jeshi la polisi wanaopata huduma za bima hasa bima ya maisha iko chini hivyo kupitia fursa hii ya shirika linakusudia kutumia mifumo ya kijeshi kuhamasisha askari kujiunga na huduma hii 

Aidha amesema jeshi la polisi litanufaika kwa kuweza kupata bei za kimakundi kwa bima ya afya ambayo ni group cover na kulingana na idadi ya ya askari na maofisa watakaojiunga na bima hiyo ambao zinaunafuu ukilinganisha na bei za kawaida za soko.

“Kwa mfano tukipata kuunga askari mmoja mpaka askari elfu 10, tutapata punguzo la asilimia 5%, tukiweza kupata askari elfu 10 mpaka elfu 20 tutapata punguzo la asilimia 7.5%, tukipata askari elfu 20 mpaka wakafika askari 30 tutapata punguzo la asilimia 10% kutoka bima yeu hii na tukipata askari zaidi ya elfu 30 tutapata punguzo la asilimia 12% “. Amesema Bw.Ruvumbagu.

Amesema kupitia fursa hiyo kutawezesha askari wetu kujiunga katika huduma kwa bei rafiki iwapo kundi kubwa litahamasika.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages