Adeladius Makwega,Safarini Kisaki – WHUSM
Serikali imesema kuwa itaendelea kuboresha huduma ya usafri kwa Watumishi wa Umma katika Mji wa Serikali kuingana na fedha zinazopatikana, kubwa kuhakikisha watumishi wanafika kazini kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali watu wa Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Bernad Marcelline mapema leo wakati akiendelea na mafunzo bora ya uwajibikaji kazi na ujazaji bora wa fomu za Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathimini ya Utendaji kazi (OPRAS) Mtumba Mji wa Serikali Jijini Dodoma.
“ Ni kweli kwa muda mrefu tumekuwa na changamoto ya usafiri wa kuwarejesha nyumbani ila kwa sasa tumepata basi kubwa na tunaamini litasaidia sana kufika kazini kwa wakati pia na kurudi nyumbani kwa wakati mjiandae na utendaji kazi wa siku inayofuata.” Alisema Mkurugenzi Marcelline.
Tunatambua kuwa ari ya kazi lazima iongezeke, kila idara na kila kitengo kinapaswa kufanya kazi kwa juhudi kwani kwa sasa kupanda mabssi ya idara na wizara nyengine itakuwa kwa kupenda tu aliongeza kiongozi huyo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Ni wajibu wa kila mtumishi sasa kuongeza juhudi ya kazi, kuwahi kazini na sasa tumehamia katika mfumo wa kidigitali na suala la kusaini kwa kutumia madaftari tumeliweka kando, lazima na kazi zetu zifanyika kwa kidigitali aliongeza.
Wakizungumza katika mafunzo hayo yanayaotarajiwa kumalizika Julai 30, 2021 watumishi wa wizara hii wamesema kuwa wanashukuru sana kupatikana kwa basi hilo ambalo limekuwa mkombozi wao kwani watumishi wengi wanakaa mjini hivyo wataweza kufika kazini kwa haraka na itapunugza gharama za usafiri.
“Kwa mtumishi anayekaa kisasa anaweza kutumia zaidi ya shilingi 6000/= kwa siku kwa kwenda na kurudi kazini. Ukitambaua kuwa hakuna usafiri wa moja kwa moja hadi Mji wa Serikali kwa hiyo atapanda hiace alafu atapanda bodaboda kwa hiyo ni gharama kubwa sana.”Anasema Julius Mgaya ambaye ni mtumishi wa kutoka Idara ya Sera na Mipango ya Wizara hii.
Mafunzo hayo yalihimishwa kwa tahadhari ya Korana kwa watumishi wakiwa ndani ya basi lao kwa kuhakikisha abiria wote wanakaa katika siti, kusimama katika vituo maalumu vya kushuka watumishi tu, kila mtumishi kuvaa barakoa akiwa ndani ya basi, watumishi kuzingatia muda wabasi linapofika katika kituo chake na mwisho watumishi kutoa ushirikiano kwa dereva wakiwa ndani ya basi hilo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇