LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 24, 2020

'HAKUNA MKATE MGUMU KWA CHAI'😀 WABUNGE VITI MAALUM CHADEMA WAAPISHWA NA SPIKA WA BUNGE, JIJINI DODOMA, LEO

Wabunge wa viti maalum Chadema wakiwa na Spika wa Bunge Job Ndugai, baada ya Spika huyo kuwaapisha katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, leo.Orodha ya Wabunge hao ni 1. Halima Mdee, 2. Grace Tendega, 3. Ester Matiko4. Cecilia Pareso,  5. Ester Bulaya,  6. Agnesta Kaiza,  7. Nusrat Hanje,  8. Jesca Kishoa,  9. Hawa Mwaifunga, 10. Tunza Malapo,  11. Felister Njau,  12. Naghenjwa Kaboyoka,  13. Sophia Mwakagenda, 
14. Kunti Majala,  15. Stela Fiayo
16. Anatropia Theonest,  17. Salome Makamba,  18. Conchesta Rwamlaza,  19. Asia Mohammed.

CCM Blog, Dodoma
Sitaki nataka' ya Chadema hatimaye imeishia ukingoni baada ya Wabunge wake 19 wa Viti Maalum Chadema kuapishwa na Spika wa Bunge,  Job Ndugai katika Viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.

Baadhi ya walioapishwa ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chadema lakini akashindwa vibaya na Mbunge wa sasa katika jimbo hilo kwa tiketi ya CCM Askofu Josephat Gwajima, katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Mbali na Halima Mdee ambaye amelazimika kurejea Bungeni kupitia kapu hilo la viti maalum, ni Grace Tendega, Esther Matiko, Jesca Kishoa na Ester Bulaya.
Endelea kufuatilia Blog hii ya Taifa ya CCM kwa taarifa zitakazojiri zaidi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages