LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 17, 2020

UCHAPAKAZI WA LUKUVI UNAMWEZESHA KUGOMBEA JIMBO LOLOTE TANZANIA NA AKASHINDA KWA KISHINDO-ASAS

 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (NEC), Salim Asas akimkabidhi Kitabu cha Utekelezaji  Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Mgombea Ubunge Jimbo la Isimani, William Lukuvi wakati wa uzinduzi wa  kampeni za uchaguzi uliofanyika Migori jimboni humo Septemba 16,2020.

Asas amesema kwa uongozi thabiti na wenye uzalendo wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. Magufuli sababu ziko wazi kwa wana Isimani na watanzania kwa ujumla kumpigia kura nyingi Oktoba 28, 2020.

Pia kwa uchapakazi wa kizalendo kwa Tanzania alionao Mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Lukuvi, anaweza kwenda kugombea jimbo lolote Tanzania na akashinda kwa kishindo, hivyo aliwaomba wana Isimani kumpigia kura nyingi.. 

Naona nisiendelee kuharibu huu uhondo, bali nawaomba muendelee kutazama na kusikiliza kwa makini yanayozungumzwa juu ya wagombea hao wa CCM kupitia kwenye video....
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (NEC), Asas akimnadi kwa wananchi mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Isimani, William Lukuvi na wagombea udiwani wa chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo.
Sehemu ya umati wa watu uliofurika kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni mjini Migori.


Lukuvi (kulia), akiwatambulisha wagombea udiwani wa chama hicho
Siku hiyo kulikuwa na burudani za kumwaga kutoka kwa wasanii mbalimbali maarufu akiwemo Harmonize.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages