Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam
Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam
Timu ya wafanyakazi wa I&M Benki walipozindua klabu yao ya michezo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, Maktaba Square jijini Dar es salaam
...............................................................................
Siku ya ijumaa tarehe 11 Septemba 2020, benki ya I&M Tanzania ilizindua klabu ya michezo kwaajili ya wafanyakazi wake kupitia kamati yake ya mabadiliko ya kitamaduni ambapo wamedhamiria kuongeza ari kwa wafanyakazi wake kwa njia ya michezo mbalimbali ikiwemo mbio fupi za riadha ambazo hufanyika kila wiki pamoja na michezo mingine kama vile gofu, mpira wa miguu, mpira wa kikapu na mpira wa mikono.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja alisema, “Tumeamua kuanzisha klabu hii ili kuhamasisha wafanyakazi wetu kuwa na afya bora, kuchangamka kiakili na kuongeza mapato kwenye benki yetu kwani wafanyakazi watakua na uwezo maradufu wa kufikiria mbinu mbalimbali za kuongeza biashara.”
Viongozi wa klabu hiyo ambao ndio walisimama kidete kuhakikisha timu ya wafanyakazi imeweza kushiriki kikamilifu katika riadha ambayo ndio ilifungua dimba la klabu hiyo, Bi Anitha Pallangyo, Meneja wa masoko na mawasiliano wa Benki ya I&M na Bi. Juliana Mtei Meneja wa kitengo cha fedha walifurahia uzinduzi huo na kuongeza kuwa wana mipango mingi kupitia klabu hiyo kuhakikisha jina la Benki ya I&M linang’ara hasa kwa upande wa michezo.
Timu ya wafanyakazi wa Benki ya I&M wakiongozwa na Mkurugenzi wa benki hiyo Baseer Mohammed walifanya riadha fupi kutoka makao makuu ya benki hiyo kwenda viwanja vya coco beach pamoja na kurudi wakiwa wamevailia jezi za michezo za klabu hiyo ikiwa ni moja ya michezo ambayo imedhamiria kuimarisha afya za wafanyakazi.
Bw. Baseer Mohammed akiongea na mwandishi wetu alisema, “Najivunia sana kuwa na timu shupavu iliojaa vijana wenye nguvu na maarifa, pia wenye uthubutu wa kuipeleka benki kwenye levo nyingine kwa kuitangaza kupitia sekta ya michezo. Faida ya michezo kwa wafanyakazi ni pamoja na kuamsha ari ya kufanya kazi, kupunguza mawazo, kuongeza ufanisi wa akili, kuamsha timu pamoja na kuongeza mahusiano mazuri kazini.
Benki ya I&M pia imetajwa kuwa ni benki bora yenye nguvu nchini Kenya ambapo imeonekana ikiwa na fursa kubwa za ukuaji pamoja na kutengeneza faida zaidi. Benki ya I&M kwa sasa ipo Tanzania, Kenya (makao makuu), Rwanda, Mauritious (Bank One) na hivi karibuni Uganda.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇