Na Yassir Simba, Globu ya jamii
MOJA
ya Wanzania ambao walipata nafasi ya majina yao kusikika na kutamba kwa
kiwango kikubwa katika medani ya mchezo wa kikapu nchini Tanzania basi
ni pamoja na kijana Hasheem Thabeet. Ndio, Hasheem alitikisa katika
mchezo huo. Watanzania wakamjua, Afrika Mashariki ikamuelewa na Dunia ya
mchezo huo ikamfahamu yeye na uwezo wake. Alikuwa na kipaji cha hali ya
juu kilichoendana na bahati.
Kwa
Hasheem Thabeet kwake haikuwa kazi ngumu kwenda nchini Marekani kwenye
ligi bora kabisa ya mchezo huo. Yaani kwa uwezo aliokuwa nao alitoka
Sekondari ya Makongo jijini Dar es Salaam na kisha kutua katika Ligi ya
NBA. Kabla ya kuendelea zaidi, naomba nieleze kidogo kuhusu NBA na kisha
tutaendelea na kile ambacho kimenisukuma kumuelezea Hasheem Thabeet.
Iko
hivi Juni mwaka 1946 katika Jiji la New York nchini Marekani ilianziswa
ligi ya mpira wa kikapu maarufu duniani ikatambulika kama NBA (National
Basketball Association), ikishirikisha timu kama Los Angeles Lakers na
Golden State Warriors. Timu nyingine ni Indiana Fever, Chicago
Sky,Phoenix, Minnesota Lynx,Los Angeles Sparks,Chicago Bulls,Miami heat
na nyengine kibao. Unapozungumzia NBA kwenye mchezo huo maana yake
unazungumzia ligi yenye umaarufu mkubwa duniani na ndio yenye mastaa
kibao.
Hivyo
Hasheem naye alikuwa moja ya mastaa kwenye ligi hiyo. Hakuwa wa kawaida.
Taarifa za Hasheem kuwamo kwenye NBA zilimsisimua kila Mtanzania.
Tulijiona wenye bahati ya hali ya juu. Sasa tuendelee, mwaka 2009,
Hasheem Thabeet aliyekuwa nyota wa mpira wa kikapu kutoka Tanzania
alisimama katika majukwaa ya uwanja Allen County War Memorial Coliseum
ya klabu ya Fort Wayne Mad Ants na kusalimiana na umati mkubwa wa
takribani mashabiki 130000 uliojitokeza usiku huo. Usiku huo ulikuwa na
maana kubwa katika mchezo wa kikapu hasa kwa wachezaji a Tanzania
wakiwamo waliokuwa wanacheza na Hasheem.
Ndio
usiku ambao ulifufua matumaini ya wachezaji wa mpira huo kwamba
inawezekana. Kama Hasheem amekwenda nao iko siku watakwenda NBA.
Watanzania wakawa wanafuatilia NBA na hasa siku ambazo timu ya Hasheem
ilikuwa inacheza. Ndiko ambako na sisi wengine tukawafahamu hao mastaa
wa Ligi hiyo achilia mbali wa Michael Jordan, William Athony Parker na
Cobe Brayant. Hata hivyo katika ligi ya NBA Hasheem Thabeet alidumu kwa
miaka mtano tu. Wakati anajiunga na ligi hiyo alitabiriwa makubwa lakini
ikawa kinyume chake. Ukweli uko hivi uwezo wa Hasheem Thabeet ulianza
kupungua kabla ya muda huo. Ziko sababu nyingi za kufanya vibaya.
Kwa
leo naomba nitaje mbili na zikibaki siku nyingine tukipata nafasi.
Sababu ya kwanza inatajwa kuwa ni utovu wa nidhamu na sababu ya pili ni
ile ya kutumia muda mwingi kwa maisha yake binafsi kuliko mchezo, sababu
zilizoainishwa na Kocha wake Damon Stoudamire kupitia mtandao wa BR MAG.
Wakati uwezo wake unaanza kupungua aliondolewa kwenye timu ya Wayne
kwenda Indiana na huko nako hali haikuwa shwari kwake. Mengi yakaanza
kuzungumza dhidi yake na mashabiki na wapenzi wa mchezo huo.
Tunafamu
Hasheem alianza kuwika kwenye mchezo huo akiwa na umri wa miaka 15.
Ilifika hatua Hasheem akawa analalamikiwa kwa kutopokea simu za muhimu
alizokuwa anapigiwa na viongozi wa timu yake. Hakuwa anajali kabisa na
matokeo yake akakumbwa a kashfa ya utovu wa nidhamu.
Kwa
sasa Hasheem Thabeet bado yupo nchini Marekani lakini sio tena kwenye
ule ulimwengu wa mchezo huo. Hasikiki tena na hakuna anayefuatilia
kutaka kujua anafanya nini. Najua huu si wakati wa kuendelea kumtupia
lawama Hasheem huenda kuna mambo yaliyomsibu hadi kufika hapo
alipofika.
Iko siku atasimulia mwenyewe.
Hata
hivyo kuna mambo ya kujifunza. Ukiwa na kipaji hasa kwenye ulimwengu wa
michezo, tambua kwamba kweli unacho kipaji na jinsi gani utahakikisha
unakilinda. Ni maoni yangu Hasheem alitambua anacho kipaji lakini
alishindwa kukilinda. Ametamba katika kipindi kifupi sana.
Nidhamu
nayo ni muhimu katika eneo lolote lile. Iwe kwenye michezo ama kazi
nyingine yoyote.Hasheem aliondoka mwenye nidhamu akiwa Makongo na baada
ya kufika NBA nidhamu haikuwa kitu chenye kipaumbele kwake.Sitaki
kumzungumiza Mbwana Ally Samata.Wengi wanasema kuhusu Samatta na kiwango
chake kwenye soka. Alibaini anacho kipaji na jukumu lake imebaki
kulinda kipaji chake na kuheshimu misingi ya soka.
Naona
kuna tofauti kubwa kati ya Hasheem Thabeet na Mbwana Samata. Tujifunze
kwa Hasheem na kisha tutafakari safari ya Mbwana Samatta.Sote
tunajivunia mafanikio ya Samatta. Tuiangalie safari yake kisha tuangalie
tumesimama upande upi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇