Charles James, Michuzi TV
DAKIKA
300 zimetosha kutumika na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
nchini (TAKUKURU) kumhoji aliyekua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe
Kangi Lugola juu ya tuhuma zinazomkabili.
Mbunge wa Jimbo la Mwibara mkoani Mara, Kangi aliwasili
katika ofisi za TAKUKUR saa 1:24 asubuhi ya leo jijini Dodoma huku
akiwa na ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kama ilivyo kawaida yake.
Mwingine
ambaye amefika kuhojiwa na TAKUKURU ni aliyekua Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi hivi
karibuni na Rais Dk John Magufuli.
Baada
ya kumaliza kuhojiwa Lugola aliondoka na gari yake aina ya Land Cruiser
VX huku akiwaeleza wandishi wa habari kuwa ni mzima wa afya.
" Mimi
sijambo, ni mzima wa afya. Kwa leo siwezi kuongea chochote," hizo ni
baadhi ya kauli za Lugola kwa wandishi wakati akitoka nje baada ya
kumaliza mahojiano.
Lugola,
Meja Jenerali Kingu na aliyekua Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto, Thobias
Andengenye wanahojiwa na TAKUKURU kufuatia kashfa ya watendaji wa wizara
hiyo kutia saini makubaliani ya zabuni ya kununua vifaa vya zimamoto
vyenye thamani ya Euro Milioni 408 sawa na Shilingi Trilioni Moja bila
kufuata utaratibu wa sheria.
Aliyekua
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoka nje ya ofisi za
TAKUKURU baada ya kumaliza kuhojiwa juu ya tuhuma zinazomkabili.
Aliyekua
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akipanda kwenye gari
yake tayari kwa kuondoka baada ya kumaliza kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa leo jijini Dodoma.
Aliyekua
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto, Thobias Andengenye akiwasilia kwenye Ofisi
za Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU
mchana huu tayari kwa mahojiano juu ya tuhuma zinazomkabili.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇