MAAFISA
Forodha wawili na aliyekuwa askari Polisi wa kituo cha Osterbay
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi
ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matano likiwemo shtaka la utakatishaji
fedha wa sh. Milioni 57.
Mashtaka
mengine wanayokabiliwa nayo ni, kuongoza genge la uhalifu, kujipatia
fedha isivyo halali, kujivika uhalisia usio wao, kutumia madaraka vibaya
na kutakatisha fedha.
Katika
hati ya mashtaka iliyosomwa na wakili wa Serikali Mkunde Mshanga
akisaidiana na Gloria Mwenda imewataja washtakiwa hao kuwa ni Edgan
Foluba (Ofisa Forodha Mwandamizi), Elizabeth Mohamed (Ofisa Forodha
Msaidizi), Victor Gama (dereva) askari polisi, PC Seleman Lusonzo pamoja
na Mohamed Mlingo na Mrisho Kamba,
Imedaiwa
mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu kuwa katika tarehe
isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es salaam washtakiwa wote kwa pamoja
walikaa na kupanga genge la uhalifu na kusababisha kujipatia shilingi 57
milioni kwa njia isiyo halali
Katika
shtaka la pili washtakiwa hao wanadaiwa, Januari 2,2020 huko katika
Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam kwa pamoja walikula njama na
kujipatia fedha kutoka kwa Harubu Abdalha wakimdanganya kuwa
watamsaidia kubadilisha fedha zake kwenda kwa Mkuu wa Mkoa na kuwa
halali.
Aidha
katika shtaka la tatu inadaiwa siku na mahali hapo, mshtakiwa Mohamed
Abdala na Mrisho Hassan katia eneo walijitambulisha kuwa ni maofisa wa
serikali wanaotoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na Mamlaka ya Mapato
(TRA) huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.
Katika
shtaka la nne la matumizi mbaya ya madaraka washtakiwa, Foluba,
Elizabeth na PC Lusonzo wanadaiwa Januari 2,mak.huu, wakiwa ni watumishi
wa umma walijipatia kiasi cha Sh. milioni 57 kutoka kwa Haroub Abdallah
wakimdanganya kuwa watampeleka kwa Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa ahadi
ya kumsaidia kubadilisha fedha haramu kosa walilolitenda Januari 2,
2020.
Washtakiwa
wote hao poa wanadaiwa kuwa, wakiwa wamedhamiria kujipatia Sh milioni
57 kutoka kwa Haroub Abdala walotakatisha fedha hizo wakijua wazi kuwa
ni zao la fedha zilizopatikana kwa njia ya udanganyifu.
Hata
hivyo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo
kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu
uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa Mahakama Kuu au mpaka DPP
atakapoipa mahalama kibali cha kuweza kuisikiliza.
Kwa
mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado
haujakamilika na itatajwa tena mahakamani hapo Januari 13, 2020.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇