Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka (katika) akiwa na mwekezaji kutoka Uturuki,Bw. Mustafa Albayram (mwenye shati jeusi) pamoja na maafisa wa serikali pamoja nabaadhi ya wafanyakazi wakitembea ndani ya kiwanda cha kuchambua pamba chaAlliance Ginnery Ltd mkoani Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akioneshwa pamba inavyochambuliwa na
mwekezaji kutoka Uturuki, Bw. Mustafa Albayram (mwenye shati jeusi).
********************************
Na Mwandishi Wetu, Simiyu
Katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania nchini Uturukiumeambatana na wawekezaji kutoka nchini humo kwa ajili ya kuwekeza katikaviwanda mkoani Simiyu ambavyo vinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 2000.
Uwekezaji
huo utajumuisha kiwanda cha nguo pamoja na kiwanda cha kutengeneza
vyombo vya majumbani ambao una thamani ya dola za kimarekani milioni 50.
Viwanda hivyo vitajengwa katika eneo la Isanga Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu na vinatarajiwa kuanza uzalishaji mwaka 2020.
Akizungumza
na vyombo vya habari katika eneo ambalo linatarajiwa kujengwa viwanda
hivyo mkoani Simiyu, mwekezaji huyo kutoka Uturuki, Bw. Mustafa Albayram
ameahidi kujenga viwanda viwili kimojawapo kikiwa ni cha nguo na
kingine cha kutengeneza vyombo vya nyumbani ikiwemo vikombe, sahani na
glasi.
Bw. Albayram amesema ameridhishwa na mazingira ya uwekezaji baada ya
kutembelea maeneo mbalimbali kwa lengo la kuangalia mazingira wezeshi kwauwekezaji wa viwanda, akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo mkoani Simiyu.
Aidha
ameitaka serikali kutatua baadhi ya changamoto ili kuuwezesha uwekezaji
huo kufanyika ikiwa ni pamoja na miundombinu yote muhimu hususani ya
umeme ili uwekezaji huo uanze mara moja baada ya kukamilisha taratibu
zote muhimu zinazohitajika ikiwa ni pamoja na usajili wa kampuni na
kutafuta hati miliki ya ardhi.
“Tumeamua
kuwekeza Simiyu, kila kitu kikienda sawa kiwanda cha nguo kinaweza
kujengwa na kufanya kazi ndani ya miezi tisa mpaka mwaka mmoja, kiwanda
cha vyombo vya nyumbani miezi nane baada ya usajili wa kampuni nitarudi
tena Simiyu kukamilisha masuala ya hati miliki ya ardhi, sitaki
kumuangusha Mhe. Balozi maana amefanya mengi kwa ajili yetu,” alisema
Albayram.
Nae
Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo amesema
mwekezaji ameridhishwa na eneo hilo na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa
Simiyu kwa kutoa ardhiya kujenga viwanda hivyo huku akibainisha kuwa ombi kubwa la mwekezaji niupatikanaji wa nishati ya kutosha kwa kuwa viwanda hivyo hutumia umeme mwingi.
Balozi
Kiondo ameongeza kuwa, hayo ni matokeo ya utekelezaji wa diplomasia ya
uchumi kwa vitendo, hivyo Ubalozi utaedelea kuhamasisha wawekezaji
wengine zaidi kuja kuweza nchini, hatimaye kufanikisha azma ya uchumi wa
viwanda.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alimhakikishia
mwekezaji huyo upatikanaji wa mahitaji yote muhimu na kuahidi
kushirikiana na taasisi za Serikali zinazohusika kuhakikisha anapata
huduma zote kwa wakati na pasipo urasimu wowote.
Kuhusu
suala la Umeme Mtaka amesema katika Bajeti ya mwaka 2019/20 Wizara ya
Nishati kupitia Shirika la umeme TANESCO imetenga fedha kwa ajili ya
ujenzi wa kituo cha kupozea umeme (substation) ambacho kitajengwa karibu
na eneo la uwekezaji huo.
Mtaka
ameongeza kuwa mtazamo wa mkoa wa Simiyu ni kuwa na viwanda vichache
vitakavyoajiri maelfu ya watanzania badala ya kuwa na viwanda vingi
vinavyoajiri watu wachache ili kuwezesha watanzania wengi kupata ajira.
Wakati
huohuo, Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa wakulima wa pamba kulima pamba kwa
wingi kwa kuwa kiwanda cha nguo kitakuwa mkombozi wa kuongeza thamani
ya zao la pamba na itauzwa kwa bei ya uhakika.
Naye
Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini, Bw. Boaz Ogola amesema
kujengwa kwa kiwanda cha nguo mkoani Simiyu kutasaidia wakulima wa pamba
kupata soko la uhakika kuondoa changamoto ya bei ya pamba kwa kuwa
kitapanua wigo wa soko la pamba, ambapo pamba inayotumika ni chini ya
asilimia 20 – 25 ya pamba yote inayozalishwa nchini.
Katika tukio jingine kampuni ya Kawasaki Heavy Industries Ltd kutoka Japanimeonesha nia ya kuanzisha kiwanda nchini ambapo kiwanda hicho kitahudumia soko la Afrika na Nje ya Afrika.
Kawasaki
Heavy Industries Ltd ni kampuni nchini Japan ambapo imewekeza katika
sekta mbalimbali kama vile sekta ya usafiri (anga, reli na majini)
nishati (cogeneration, energy plants, gas tuibines, gas engines), vifaa
vya viwandani (hydraulic components and systems, robotics, industrial
plants, environmental and recycling), pamoja na leisure (motorcycle,
off-road four wheel,JET SKI).
Naibu
Meneja wa Idara ya Mkakati wa Kimataifa, Kitengo cha Biashara cha
Kampuni ya Kawasaki Bw. Michio Kambe anatarajia kufanya ziara nchini
Tanzania kuanzia tarehe 21 hadi 26 Novemba 2019 ambapo atakutana na
kufanya mazungumzo na Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Ofisi ya Waziri Mkuu
– Uwekezaji na Waziri wa Viwanda na Biashara.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇