LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 3, 2025

JAJI MWAMBEGELE AWATAKA WAZALISHAJI WA MAUDHUI MTANDAONI KUWAFIKISHIA WANANCHI TAARIFA SAHIHI ZA UCHAGUZI

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele  amesema kwa muktadha wa kufanikisha vyema Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Tume inawatambua na kuwategemea Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kwa jukumu kubwa la kufanikisha upatikanaji wa habari sahihi kwa haraka na kwa wigo mpana, zinazolenga hasa makundi ya vijana na watu wanaotumia teknolojia ya kidijitali kwa wingi.


Jaji Mwambegele ameyasema hayo akifungua Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na wazalishaji wa maudhui mtandaoni kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam Agosti 3, 2025.

"INEC, inawategemea kuendesha kampeni za uhamasishaji mitandaoni kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na michoro, video na ujumbe unaolenga kuvutia makundi tofauti ya wapiga kura, hasa vijana na watu wanaotegemea teknolojia kupata habari," amesema Jaji Mwambegele.

"Tume inathamini sana  mchango wao katika kuandaa, kuchapisha na kusambaza taarifa kupitia majukwaa ya kijititali kama mitandao ya kijamii, blogu, tovuti na majukwaa ya picha jongefu kama YouTube," ameongeza Jaji Mwambegele.

Aidha, Jaji Mwambegele amewashukuru kwa namna ambavyo wamekuwa wakiipatia Tume hiyo ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2025.

Ametumia fursa hiyo kuwaomba kuendelea kushirikiana na Tume na kutumia nafasi zao kwa jamii kwa kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya uchaguzi mkuu na kua hamasisha wananchi waliojindikisha kwanye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wajitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amewahimiza waandishi hao kutumia kalamu na nyenzo zao kueneza ujumbe wa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi, ili kulinda mshikamano wa kitaifa na kuimarisha misingi ya demokrasia.

 

Pia amewaasa kuepuka kuchapisha au kurusha habari zinazoweza kuwavunja moyo wananchi na kuwafanya waone kama hakuna umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi, iwe ni kama wapiga kura au wagombea.

 

Mkutano kati ya Tume na wadau hao wa habari za mitandaoni ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya wadau mbalimbali ambayo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikiitisha katika maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

 

Mikutano hiyo ilianza tarehe 27 Julai 2025 kwa kukutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa, ikafuatiwa na mkutano na Wawakilishi wa Asasi Zisizo za Kiserikali kisha Wawakilishi wa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari.

 

Mfululizo huu wa mikutano unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 4 Agosti 2025, baada ya mkutano na Waandaji wa Maudhui Mtandaoni, utakaofuatiwa na mafunzo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari.





Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, akifungua Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na Wazalishaji wa maudhui mtandaoni kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, uliofanyika  Agosti 3, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza wakati wa kuwasilisha mada katika mkutano wa Tume na Wazalishaji wa maudhui mtandaoni  kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. 
Makamu Mwenyekiti wa INEC, Jaji mstaafu Mbarouk S. Mbarouk akizungumza wakati wa kufunga semina hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu kwa Umma, Giveness Aswile akitoa neno la utangulizi alipokuwa akimkaribisha Mkurugenzi wa Huduma za Habari wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Andrew Kisaka ambaye aliwasihi wanahabari kuwa makini kuandika habari zisizochochea vurugu hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi ili Nchi isije ikaingia katika machafuko.    

Mkurugenzi wa Huduma za Habari wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Andrew Kisaka  akiwasihi wanahabari kuwa makini kuandika habari zisizochochea vurugu hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi ili Nchi isije ikaingia katika machafuko.    

Wanahabari Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni wakiwa katika semina hiyo muhimu.






Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakiwa katika picha na viongozi wa Tume.

















 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages