Jul 29, 2019

MOI KUFANYA UPASUAJI WA UBONGO KWA TEKNOLOJIA MPYA

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile akifungua kongamano la kimataifa la upasuaji wa uvimbe wa kansa za Ubongo na uti wa Mgongo kwa kutumia teknolojia  ya kisasa MOI leo July 29, 2019. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na washiriki katika kongamano la kimataifa la upasuaji wa uvimbe wa kansa za Ubongo na uti wa Mgongo kwa kutumia teknolojia  ya kisasa MOI leo July 29, 2019.
 Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamnini MOI Prof. Charles Mkony akizungumza katika kongamano la kimataifa la la upasuaji wa uvimbe wa kansa za Ubongo na uti wa Mgongo kwa kutumia teknolojia  ya kisasa MOI leo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa taarifa ya utendaji wa MOI katika kongamano la kimataifa la la upasuaji wa uvimbe wa kansa za Ubongo na uti wa Mgongo kwa kutumia teknolojia  ya kisasa MOI leo.
 Washiriki wa kongamano la Kimataifa la upasuaji wa uvimbe wa kansa za Ubongo na uti wa Mgongo kwa kutumia teknolojia  ya kisasa wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii Dkt Faustine Ndugulile leo.
 Dkt Ryan Ormond kutoka chuo kikuu cha Colorado cha nchini marekani akiwasilisha mada katika kongamano la kimataifa la upasuaji wa uvimbe wa kansa za Ubongo na uti wa Mgongo kwa kutumia teknolojia  ya kisasa MOI leo.
 7.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile watatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja Uongozi wa MOI, wajumbe kutoka chuo Kikuu cha Colorado pamoja na washiriki wa kongamano la kimataifa la upasuaji wa uvimbe wa kansa za Ubongo na uti wa Mgongo kwa kutumia teknolojia  ya kisasa MOI leo.
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Faustine Ndugulile (MB) akizungumza jambo katika kongamano hilo

Dar es Salaam, 29/07/2019. Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Faustine Ndugulile (MB) leo amefungua kongamano la kimataifa la mafunzo ya upasuaji wa uvimbe wa kansa za Ubongo na uti wa Mgongo kwa kutumia teknolojia  ya kisasa.

Dkt. Ndugulile amesema kongamano hilo linahusisha mbinu za kisasa za upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo kwa kupitia kwenye tundu la pua, upasuaji wa ubongo kwa njia ya matundu na matumizi ya kifaa cha ultrasound wakati wa upasuaji wa ubongo ambapo  limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya MOI na Chuo Kikuu cha Colorado cha Marekani.

“Serikali imetoa fedha Kiasi Cha Tshs Bilioni 7.9 kwa ajili ya kununua na kusimika mitambo ya kisasa ya upasuaji wa ubongo ‘Angio Suite’ tunaamini kabla ya mwisho wa mwaka itaanza kazi maana wataalamu wapo tayari ambao Serikali iliwapeleka nchini China kupata mafunzo hayo” Alisema Dkt Ndugulile

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini MOI Prof. Charles Mkony ameishukuru Serikali kwa kundelea kufanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya Taasisi ya MOI jambo ambalo limepelekea huduma kuendelea kuwa za kiwango cha juu na kumaliza rufaa za nje ya nchi.
Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema mchakato wa kununua na kufunga maabara ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo ijulikanayo kama ‘Angio Suite’ utakamilika kabla ya mwezi oktoba ambapo huduma zitaanza kabla mwaka huu haujaisha.

“Kuanza kwa huduma hizi za upasuaji wa ubongo kwa teknolojia ya kisasa kutaleta mageuzi makubwa kwenye utoaji huduma za Upasuaji wa ubongo kwenye ukanda huu wa Afrika mashariki na kati kwani hakutakua na haja kwa wagonjwa kuzifuata huduma hizo nje ya nchi, utakua upasuaji ambao unahusisha kupitia kwenye mishipa ya damu hadi kwenye ubongo na kurekebisha tatizo bila kufungua fuvu” Alisema Dkt Boniface
Kongamano hili linahudhuriwa na zaidi ya madaktari 100 kutoka katika mataifa ya Kenya, Uganda, Rwanda, Sudani, Ethiopia pamoja na mataifa mengine kutoka kwenye nchi za Afrika mashariki ,kati na kusini.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano MOI

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages