Jul 3, 2025

DAKTARI BINGWA WA UPASUAJI WA UBONGO, ALHAJ DK. MZIMBIRI ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MLALO

Daktari Bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (Neurosurgeon) katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Alhaj Dk. Juma Magogo Mzimbiri, amejitosa kuwania Ubunge jimbo la Mlalo mkoani Tanga, akieleza lengo lake kuwa ni kuongeza wigo wa kuihudumia jamii.

Alhaj Dk. Mzimbiri kwa sasa ndiye Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Ajali (Emergency). Pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kliniki ya kibingwa  ya THE CURE iliyopo Upanga mtaa wa Mindu na Maliki jijini Dar es salaam. 

Amesomea taaluma yake nchini China, India na Marekani na amekuwa akiendesha vipindi  mbalimbali vya afya katika vyombo vya nchini kama Azam Tv na vya kimataifa kama BBC na Umoja wa Mataifa UN Tv. 

Pia Alhaj Dk. Mzimbiri ni mshindi wa tuzo za Tafiti za Kansa zilizotolewa na Waziri wa Afya Jenista Mhagama katika Hospital ya Shifaa iliyopo jijini Dar es salaam. kwa upande wa CCM, ni Mjumbe wa CCM katika tawi la Tambaza, Kata ya Upanga Magharibi jijini Dar es salaam.
Alhaj Dk. Mzimbiri akikabidhi fomu yake kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Lushoto, Miriam Kaaya jana. Katikati ni Baba yake Mzazi Idriss Abushehe Musa Mimbiri. 
Alhaj Dk. Mzimbiri akiwa na fomu yake kabla ya kuirejesha jana.

Waziri wa Afya Jenista Mhagama akimkabidhi tuzo Alhaj Dk Mzimbiri ambaye aliibuka mshindi wa tuzo za Tafiti za Kansa. hafla hiyo ilifanyika  Hospital ya Shifaa iliyopo jijini Dar es salaam.

Chini ni picha mbalimbali Alhaj Dk. Mzimbiri  akiendesha vipindi  mbalimbali vya afya katika vyombo vya Azam Tv, BBC na Umoja wa Mataifa UN Tv. 


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages