Akizungumza leo Novemba 2024 katika Viwanja vya Buliaga wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam ,CPA Makala ameeleza hatua kwa hatua sababu za wagombea waliosimamishwa na Chama hicho katika kugombea nafasi za uongozi katika vijiji, Vitongoji na Vijiji huku akisisitiza Chama Cha Mapinduzi kinayodhamana ya kuwatumikia Watanzania.
"Tunazindua kampeni za Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji nchi nzima. Ni hatua nyingine muhimu baada ya hatua mbalimbali kupita na tumepitia mchakato wa hatua mbalimbali.Vyama vya Siasa vilipewa fursa kupitia R4 za kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara,hivyo vyama vilianza maandalizi vya kueleza kuhusu uchaguzi.
"Umma wa Watanzania ulielewa kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na wote wameelewa.Chama cha Mapinduzi kimefanya kila namna ya kueleza kuhusu uchaguzi.CCM iliwaandaa Watanzania kuhusu uchaguzi huu.
"Hatua iliyoafuata ilikuwa kujiandikisha na uchaguzi wa safari hii hamasa ya kujiandikisha ilikuwa kubwa na Dar es Salaam inatajwa kuwa imefanya vizuri katika uandikishaji.Hatua nyingine ilikuwa kuandikisha wagombea nchi nzima stori ilikuwa ni wagombea wa CCM.
"CCM ndio chama chenye wanachama wengi,inayoheshimu misingi ya demokrasi lakini ni Chama kinachofanywa mambo yake kwa uwazi.Kule kwingine hakuna kura za maoni unasikia kamanda umo.CC ina utaratibu wake na ndio maana baada ya kura za maoni tumepita Wilaya zote kuvunja makundi."
Akielezea zaidi CPA Makala amesema hatua iliyoafuata ilikuwa uteuzi wa wagombea na Chama hicho kimesimamisha wagombea katika nafasi."Nawatangazia Watanzania kwamba CCM imesimamisha wagombea katika nafasi zote,hatuhitaji huruma wala mbeleko."
Amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi wakati kinazindua kampeni nchi nzima wanaaminu huo ni mkakato mwingine wa kuomba kura kwa Watanzania ili wagombea wa CCM washinde.
"Tutamia R4 za Rais kufanya kampeni,hatutaki matusi kejeli na tutafanya kampeni za kistaarabu kwasababu CCM ni Chama kiongozi lakini tuna ajenda na hoja za kuwaambia Watanzania.Asiyekuwa na hoja atafanya kampeni za kujeli na kutukana lakini sisi tutawajibu kwa hoja na Watanzania watapima nani anatakiwa kupewa kura.
UMUHIMU UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Akizungumza kuhusu umuhimu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji CPA Makala amesema uchaguzi huo ndio maisha yetu na kwamba viongozi wanaoenda kuchaguliwa ndio tunaishi nao,wanajua changamoto za wananchi.
"Ndio hao ndio watu ambao watatuonesha maeneo ya kujenga madarasa, vituo vya afya.Viongozi tunaokwenda kuwachagua ndio hao wanaotoa barua kwa ajili ya dhamana pale ambako yanatokea matatizo kwa baadhi yetu.Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji ni watu muhimu katika uchaguzi huu.
"Hivyo tunapokwenda kuchagua viongozi lazima tuchague viongozi ambao shughuli za maendeleo zinaanzia katika maeneo Yao kwa maana ya ngazi za chini.Wenyeviti wa Mitaa ,Vijiji na Vitongoji ndio wanaohusika na ulinzi na usalama,hivyo mnaweza kuona uchaguzi huu ni muhimu sana.
"Mafanikio yote yaliyopatikana katika maeneo mbalimbali yametokana na ushirikiano wa wenye viti wa Serikali kwani hakuna mradi ambao umetekelezwa bila ushirikiano wa mtaa.Niwasihi Watanzania wafahamu CCM imeteua wagombea wazuri .Wagombea hao ni muhimu na muwaamini,"amesma CPA Makala.
SABABU ZA KUCHAGUA WAGOMBEA WA CCM
Akitoa sababu za kuwaomba Watanzania wawachague wagombea wa CCM kwasababu Chama hicho ndio kinatekeleza Ilani ya Uchaguzi mkuu 2020-2025 ,hivyo wagombea wa CCM wakishinda wataungana na madiwani , Wabunge na Rais katika kufanikisha utekelezaji wa Ilani.
"Mbowe amesema Chadema hawana Ilani ila kila mgombea atabuni Ilani ya mtaani,kama kuna Mwenyekiti wa Kijiji abuni anachofikiria.Mtapata picha kama mnaenda katika uchaguzi kuna Chama kina Ilani halafu kuna chama kingine wagombeawa wake hawana Ilani.Niwahakikishie Watanzania tunayo safari nzuri ya kuelekea katika maendeleo na maendeleo yataletwa na CCM."
Pia amesema CCM ndio Chama chenye dhamana ya kuwatumikia Watanzania nchi nzima na kwamba vyama vingine hawana wajibu huo na kazi yao ni kufanya maandamano.
"Tunayo dhamana ya kuyasaidia makundi mbalimbali yakiwemo ya mama Lishe,bodaboda lakini wenzetu hawana Ilani wameambiwa wabuni buni tu.CCM ndio Chama pekee ambacho kikiahidi kinatenda,wenzetu hawaaminiki"
TUKAPIGE KURA NOVEMBA 27
Pamoja na hayo CPA Makala amesema ushindi wowote unatangazwa kwa kupata kura nyingi,hivyo amewaomba Watanzania wakiwemo wanaCCM tarehe 27 wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kwamba watatangazwa kushinda baada ya kupiga kura.
"Kama wote tutakwenda kupiga kura kama tulivyojiandikisha tutashinda kwa kishindo,CCM tutashinda kwa haki hatuhitaji mbeleko lakini nisisitize kila aliyejiandikisha akapige kura.Tunaamini utaratibu wa kuwa na Mawakala na ndio watalinda kura zetu pale vituoni.Tarehe 27 sio mbali,kila mmoja akapige kura."
MAAGIZO KWA KAMATI ZA SIASA
Aidha, Mwenezi Makalla ameziagiza Kamati za Siasa ngazi ya Kitongoji, Mtaa, Kata na Wilaya kuhakikisha wanasaka kura nyumba kwa nyumba na kuwanadi wagombea wa CCM.
"Leo tumezindua kampeni hapa Wilaya ya Temeke, Wilaya iweke utaratibu kufanya kazi ya kampeni kwa wagombea wa CCM, mabalozi, Kamati ya Tawi, Kamati ya Kata, Kamati ya Siasa ya Wilaya na Kamati ya Siasa ya Mkoa zifanye kazi ya kuwanadi wagombea wa CCM."
Picha Mbalimbali za Uzinduzi wa Kampene za CCM Moka wa Dar Es Salaam
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇