Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi amewataka wananchi wa Jimbo lake katika Kata zote kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili kuweza Kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuchagua viongozi bora na wanaowapenda.
Mhe. NDAKIDEMI ameyasema hayo leo tarehe 11, Oktoba 2024 wakati akizungumza na wananchi waljitokeza kujiandikisha katika Kijiji cha Boro, Kata ya Kibosho Kirima. Mbunge Ndakidemi ni mzaliwa wa Kijijiji cha Boro.
“Napenda nichukue nafasi hii kuwaomba nyie mliomaliza zoezi hili leo mkawahimize wananchi wengine kwenye familia zetu, vitongoji, kijijini na kwenye Kata na kuhakikisha wanajiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura katika makazi yao wanakoishi. Hii itawawezesha kupiga kura tarehe 27.11.2024 kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa mnaowapenda na watakao leta mafanikio katika maeneo yetu. Alisema Mheshimiwa Mbunge.
Prof. Ndakidemi akijiandikisha katika daftari hilo.Prof. Ndakidemi akiwa kwenye foleni pamoja na wananchi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇