LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2024

BALOZI NCHIMBI AKEMEA VIONGOZI WANAOJIGEUZA MIUNGU WATU , BADALA YA KUTUMIKIA WANANCHI.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Emmanuel Nchimbi, akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM wilaya ya Kahama, leo Oktoba 10 2024 akiendelea na ziara ya kuimarisha chama na kuhamasisha wananchi kuhusu kujiandikisha katika daftari la mpiga kura mkoa  wa Shinyanga

..............................

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewataka viongozi wa CCM kutenda haki kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba mwaka huu.

Akizungumza na viongozi na wanachama mbalimbali wa CCM Wilaya ya Kahama leo, tarehe 10 Oktoba 2024, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Shinyanga, akiambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla, na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Hamid Abdalla.

Balozi Nchimbi amesema kila mwanachama wa CCM ana haki sawa na mwingine, akisisitiza kuwa ni kinyume cha maadili ya CCM kumnyima mtu mwenye sifa bora nafasi ya uongozi kutokana na chuki binafsi.

“Tunakoelekea kwenye chaguzi zetu, utekelezaji wa haki unatakiwa. Acheni kupanga safu. Viongozi bora ndio wapitishwe. Ni kosa kubwa la kimaadili ndani ya CCM kiongozi kumkamia mwanachama… kwamba eti safari hii nitahakikisha fulani anakatwa kwenye chama chetu. Hiyo hapana, kwani kila mwanachama ndani ya CCM ana haki sawa na mwingine.”

“Tuna watu, ukimalizika tu uchaguzi ndani ya Chama chetu, anaanza upelelezi nani ambae hajamuunga mkono na kuanza kumshughulikia. Hiyo ni tabia mbaya na haikubaliki. Kwani mtu kukupigia kura ni haki yake, akikunyima kura ni haki yake pia. Kuna wengine viongozi wamejigeuza kuwa miungu watu. Hiyo hapana. Viongozi wazuri husambaza upendo,” amesema Balozi Nchimbi.

Katibu wa Idara ya Itikadi, Uenezi, na Mafunzo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Amos Makalla, ametoa wito kwa Watanzania na wanachama wa CCM kujiandikisha katika daftari la makazi ili kuhakikisha wanapata fursa ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Katika hotuba yake, Makalla alisisitiza kuwa zoezi hili ni muhimu kwa kila mwananchi anayependa kushiriki katika kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo ya haraka katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages