LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2024

KAHAMA MBIONI KUPATA MKOA WA KITANESCO

Kahama 

Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi Balozi Emmanuel Nchimbi akitatua kero sugu kwa wanakahama amempigia simu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko ili kufahamu utatuzi wa maombi ya wanakahama juu ya kupata Mkoa wa Kitanesco kwa sababu Umeme unakatika katika sana kwenye Maeneo yao.

Nae Mhe Dotto Biteko akijibu swali hilo kwa njia ya Simu amesema ni kweli Wabunge wa Kahama wamemuomba sana suala hilo na wamefanya mapitio katika Yale maeneo yatakayopewa Mkoa wa kitanesco basi Kahama ni namba moja.

"Tulipata maombi  kutoka kwa Wabunge wakahama, Sisi tulifanya uchambuzi mkubwa kwenye maeneo ambayo yatapata Mkoa wa kitanesco na Kahama itapata Mkoa wa kitanesco kwani tumejiridhisha na maeneo haya yana migodi ya Madini hivyo Mwaka ujao wa fedha tutajenga Mkoa wa kitanesco Kahama."

Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amezungumza na Mamia na Maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Kahama leo, tarehe 10 Oktoba 2024, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Shinyanga, akiambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla, na Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndugu Rabia Hamid Abdalla.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi, akihutubia   Maelfu ya Wananchi waliojitokeza Viwanja vya Stendi ya Malori Majengo wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 10 Octoba 2024.

Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla akizungumza na Maelfu ya Wananchi waliojitokeza Viwanja vya Stendi ya Malori Majengo wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 10 Octoba 2024.

Wanachama wa Vyama Vya upinzania wakirudisha kadi na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi katika mkutano uliofanyika Viwanja vya Stendi ya Malori Majengo wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 10 Octoba 2024.


Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdalla Hamid akizungumza na Maelfu ya Wananchi waliojitokeza Viwanja vya Stendi ya Malori Majengo wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 10 Octoba 2024.



 Maelfu ya Wananchi waliojitokeza Viwanja vya Stendi ya Malori Majengo wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 10 Octoba 2024.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages