LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 29, 2022

WAFAHAMU WALIOVUMA KWENYE VYOMBO VYA HABARI AFRIKA MASHARIKI, MANDONGA YUMO

William Ruto

CHANZO CHA PICHA,WILLIAM RUTO/TWITTER

Maelezo ya picha,

Rais Mteule wa Kenya William Ruto

Tunapoelekea kuuaga mwaka 2022 , tunaangazia orodha ya watu ambao majina yao yalitajwa sana katika vyombo vya habari na katika mitandao ya kijamii eneo la Afrika mashariki.

William Ruto- Kenya

Rais wa Kenya William Ruto aliushangaza ulimwengu baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Kenya mwezi wa Agosti licha ya mtangulizi wake Uhuru Kenyatta kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Mwanasiasa huyu tajiri ambaye amekuwa na ndoto za kuwa Rais wa Kenya, amekuwa akikutana na vikwazo lukuki vya kisiasa, ikiwemo kuzuiwa kwa sababu ama kuzuiwa kwa makusudi kufanya shughuli kadhaa za kisiasa na binafsi kutokana na msukumo wa kisiasa.

Kuwa mwanasiasa kunahitaji uwe na ngozi ngumu, lakini kuwa sehemu ya Ruto kunahitaji kuwa ngozi ngumu zaidi, ni miongoni mwa wanasiasa wachache waliopitia masaibu makubwa katika maisha yao ya siasa Kenya.

Kainerugaba Muhoozi- Uganda

Luteni Jenerali Kainerugaba Muhoozi anadaiwa kupikwa ili amrithi baba yake Yoweri Museveni uraisi wa Uganda
Maelezo ya picha,

Jenerali Kainerugaba Muhoozi anadaiwa kupikwa ili amrithi baba yake Yoweri Museveni uraisi wa Uganda

Mtoto mkubwa wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni kamanda wa jeshi la ardhini nchini humo Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, aligonga vichwa vya habari mwaka huu kutokana na machapishoyake tata yaliyozua hisia kati katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Kauli yake ya tarehe 2/10/2022 ya kudai kwamba majeshi yake yangeliweza weza kuteka kuiteka Nairobi ndani ya wiki mbili tu'

yalizua hisia mseto miongoni mwa Wakenya mtandaoni maarufu kama KOT ambao walilitaka jeshi lake kwanza kumkamata kiongozi wa waasi na mbabe wa kivita Joseph Kony kabla ya kuiteka Kenya huku wengine wakimuunga mkono na kudai kwamba jeshi la Uganda lipo imara zaidi ya majeshi yote Afrika Mashariki.

Hatahivyo serikali ya Uganda baadaye ilitoa taarifa ikikana machapisho ya jenerali Muhoozi ikisema kuwa yalikuwa ya kibinafsi.

Jenerali huyo pia aliwaomba msamaha Wakenya akiseama kwenye chapisho lingine: "Siwezi kulipiga jeshi la Kenya kwa sababu baba yangu aliniambia nisijaribu kamwe! Kwa hiyo watu wetu nchini Kenya wanapaswa kutulia!" Jenerali Kainerugaba alitweet.

Ferdinand Omanyala -Kenya

Ferdinand Omurwa Omanyala

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ferdinand Omanyala

Mwanariadha wa Kenya wa mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala mwaka huu aliushangaza ulimwengu baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya nchi za Jumuiya ya Madola mjini Birmingham Uingereza.

Omanyala aliyeandakisha muda wa sekundÄ™ 10.02 aliipatia Kenya medali yake ya kwanza ya dhahabu katika mashindano hayo baada ya kumshinda bingwa mtetezi wa mashindano hayo Akani Simbine kutoka Afrika kusini aliyechukua nafasi ya pili.

Yupun Abeykoon kutoka Sri Lanka alimaliza wa tatu na hivyobasi kujipatia medali ya shaba kwa kumaliza katika muda wa sekunde 10.14.

Ushindi huo wa Omanyala ulimweka katika vitabu vya kumbukumbu kama mwanariadha wa kwanza Mkenya katika miaka 60 kumaliza wa kwanza katika mbio za mita 100 za wanaume katika mashindano hayo.

Mbunge Linet chepkorir

Linet

Linet chepkorir maarufu 'Toto', mwenye umri wa miaka 24 aligonga vichwa vya habari ndani na nje ya Kenya baada ya kuwapiku wagombea wengine wanane aliokuwa akishinda nao kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agost mwaka huu nchini Kenya.

Baadhi ya aliowapiku ni wanasiasa wenye uzoefu mkubwa. Linet Chepkorir ameandikisha historia ya kuwa mwanamke mwenye umri mdogo zaidi kuwa kuwa mwakilishi Bungeni.

Karim Mandonga- Tanzania

Bondia huyu wa ngumi za kulipwa kutoka Tanzania alivuma mitandaoni mwaka 2022 kutokana na jina 'ndoige' alilopatia aina ya ngumi ambayo angetumia dhidi ya bondia mwenzake kutoka mjini Morogoro Said Mbelwa.

Pambano lake la Novemba 25/11/2022 dhidi ya Said Mbelwa lilisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake kutokana na jinsi alivyosifia ndoige navile angeitumia ulingoni.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages