LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 29, 2022

LOWASSA ALAZWA AFRIKA KUSINI

Johanagasburg, Afrika Kusini

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amemwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya  Kusini.

 

Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

 

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2022) jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali Mheshimiwa Lowassa.

 

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

 

Naye mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

Edward Lowassa

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages