LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 29, 2022

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI DISEMBA 29, 2022

G

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Real Madrid itaweka kipaumbele mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham mnamo 2023, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 akitarajiwa kuchagua timu ya Hispania badala ya Liverpool. (Goal)

Bellingham atakaa na Borussia Dortmund mwezi Januari kujadili mustakabali wake. (Liverpool Echo)

Manchester City wako tayari kuwapa AC Milan kiungo wao wa kati wa muingereza Jack Grealish, 27, ili kubadilishana na mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao, 23. (Calciomercato - in Italian)

Jack

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Jack Grealish

Manchester United, Arsenal na Chelsea wana mashaka kuhusu kufikia ada ya uhamisho wa mkopo ya Atletico Madrid ya pauni milioni 8 kwa ajili ya mshambuliaji wake wa Ureno Joao Felix, 23. (Sport)

Chelsea wanavutiwa na mlinzi wa Celtic na Croatia Josip Juranovic, 27, kama mbadala wa Reece James, 23, aliyeumia. (Sky Sports)

Chelsea pia inamtazama mlinzi wa Inter Milan na Uholanzi Denzel Dumfries, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 pia akiwa kwenye rada za Manchester United. (La Gazzetta dello Sport)

Newcastle United wamefutilia mbali uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Jorginho, 31. (Football Insider)

Jorginho

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Jorginho

Arsenal wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27. (Corriere dello Sport, via Express).

Shakhtar Donetsk wanasema wanataka karibu euro 100m kwa ajili ya winga wa Ukraine Mykhailo Mudryk, 21, ambaye anaripotiwa kuuwa chaguo la kwanza la Arsenal. (Clciomercato)

Manchester United itajielekeza zaidi kusajili katika dirisha la usajili la majira ya joto mwaka ujao badala ya kutumia dirisha la Januari. (Sky Sports)

Mshambulizi wa Atletico Madrid na Uhispania Alvaro Morata, 30, anaripotiwa kusakwa kwa mkopo na Manchester United. (ESPN)

Morata

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Morata

Mchezaji mmoja kwenye orodha ya wanaosakwa na United ni mlinzi wa Napoli na Korea Kusini Kim Min-jae, 26. (Italia)

Bournemouth wameungana na Leicester City kuonyesha nia ya kutaka kumnunua winga wa zamani wa Chelsea anayekipiga Atalanta Jeremie Boga, huku raia huyo wa Ivory Coast, 25, akipatikana kwa mkopo. (Maiil)

Leeds wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsaini nahodha wa RB Salzburg na mlinzi wa Austria Maximilian Wober, 24, lakini Everton pia wanamtaka. (Fabrizio Romano, via TeamTalk)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages