|
Diwani wa Kata ya Kawe Mutta Rwakatare akifanya uzinduzi wa Shina la Wakereketwa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Tawi la Kibomu katika Kata hiyo, jana. Kushoto ni Katibu wa UVCCM tawi la Kibomu Abdulkareem Jamal na Mwenyekiti wa UVCCM Tawi hilo Eliyas John Komba na Kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kibomu Steven Kinyota. |
|
|
Diwani Rwakatare akipokewa na Katibu wa CCM Tawi la Kibomu Pili Mussa alipowasili kwa ajili ya kufanya uzinduzi wa Shina hilo la wakereketwa wa UVCCM Tawi hilo la Kibomu. Katikati ni Katimu Mwenezi wa CCM Kata ya Kawe Potipoti Ndanga
|
|
Diwani Rwakatare akikumbatiwa kwa furaha na Katibu Pili Mussa katika mapokezi hayo.
|
|
Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Kibomu akimlaki Diwani Rwakatare baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Tawi la Kibomu.
|
|
Kisha Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Kibomu akamsalimia Diwani Rwakatare baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Tawi la Kibomu. |
|
Diwani Rwakatare akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Tawi la Kibomu |
|
Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Kibomu akimuongoza Diwani Rwakatare na wanachama wengine wa UVCCM kwenda eneo la uzinduzi wa Shina la wakereketwa, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Tawi la Kibomu. Mtoto aliyeshikwa mkono na Diwani Rwakatare ni Potipoti mdogo.
|
|
Matembezi yakiendelea kwenda eneo la tukio Mtaa wa Kibomu.
|
|
Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Kibomu Elias John Komba akisalimia baada ya msafar wa Diwani Rwakatare kuwasili Ofisi kwenye uzinduzi wa Shina la wakereketwa wa UVCCMya CCM Tawi la Kibomu |
|
Diwani Rwakatare akisamilia na kuzungumza kabla ya kuzindua shina hilo.
|
|
Diwani Rwakatare akishirikiana na Viongozi wengine kuzindua Shina hilo la Wakereketwa wa UVCCM Tawi la Kibomu.
|
|
Diwani Rwakatare akipandisha bendera baada ya kuzindua shina hilo la Wakereketwa wa UVCCM.
|
|
"Sasa hapa safi", akasema Diwani Rwakatare.
|
|
Vijana wakiondoka kikakamavu eneo la tukio baada ya uzinduzi.
|
|
Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Kibomu Elias John Komba akimuongoza Diwani Rwakatare kwenda katika Ukumbi wa Salome Social Hall, Mbezi Kwa Komba baada ya kuwasili.
|
|
Mwenyekiti wa UVCCM
Tawi la Kibomu Elias John Komba akimuongoza Diwani Rwakatare kwenda
katika Ukumbi wa Salome Social Hall, Mbezi Kwa Komba baada ya
kuwasili. |
|
Diwani Rwakatare akiwa na viongozi wa meza Kuu baada ya kuwasili ukumbi wa Salome Social Hall kuendelea na shughuli
|
|
Diwani Mutta na meza kuu wakishangilia Mama Kapteni John Komba alipoitwa kwenda kuketi meza Kuuu
|
|
Mmliliki wa Ukumbi wa Salome Social Hall Mama Salome Kapten John Komba akipokewa na Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Kibomu Elias John Komba alipoitwa kwenda kukaa Meza Kuu. Mwenyekiti Elias ni Mtoto wa Mama Kapteni John Komba.
|
|
Mama Kapteni John Komba akikaribishwa meza kuu na Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kawe Potipoti
|
|
Mama Kapteni John Komba akikaribishwa meza kuu na Diwani Rwakatare.
|
|
"Wacha
wasemee Chama Cha Mapinduzi kina wenyewe, Wacha waseme Chama cha
Mapinduzi kina wenyeweee!" Mwenyekiti wa UVCCM
Tawi la Kibomu Elias John Komba akiimba sehemu ya wimbo huo ulioimbwa na
Marehemu Baba yake enzi za uhai wake akiongoza kundi la TOT enzi za
uhai wake.Elias aliimba kipande cha wimbo huo kabla ya kuzungumza
alipinuliwa katika utambulisho. |
|
Mwenyekiti wa UVCCM
Tawi la Kibomu Elias John Komba akiendelea kuamsha hamasa ukumbini. |
|
Diwani Mutta akimfurahia Mwenyekiti Elias alipomaliza kuimba sehemu ya wimbo huo wa CCM.
|
|
Katibu wa UVCCM Kata ya Kawe Neema Mathias akizungumza katika hafla hiyo
|
|
Mwenezi CCM Kata ya Kawe akimtambulisha Potipoti mdogo katika hafla hiyo.
|
|
Mwenezi Kata ya Kawe Ndugu Potipoti akiomba waliohudhuria hafla hiyo kusimama ili kumbuka hayati John Komba, Mchungaji Mama Rwakatare na wengine wote waliokwishatangulia mbele za haki, wakati wa hafla hiyo
|
|
Wakiwa wamesimama na kukaa kimya kwa dakika tano kuwakumbuka marehemu hao
|
|
"CCM Hoyeeee, Mama Samia hoyeee, na Diwani wetu hoyeee....", Mama Salome John Komba akasema wakati akisalimia ukumbini,
|
|
Ukumbi ukalipuka kumshangilia Mama John Komba baada ya kusalimia.
|
|
"Kwanza nitoe pole kwa tukio lile la panya road kufanya uporaji na mauaji, pale Muzimuni katika hii Kata yangu, nawaambieni tutashirikiana na vyombo vyote vya usalama na wananchi kuhakikisha kila aliyehusika anapatikana na kuchukua hatua stahiki", akasema Diwani Mutta aliposimama kuhutubia katika hafla hiyo.
|
|
Diwani Mutta akiendelea na hotuba yake.
|
|
Wakiendelea na hafla hiyo
|
|
Shangwe ukumbini.
|
|
Shangwe ukumbini.
|
|
Shangwe ukumbini.
|
|
Wadau wakiwa ukumbini.
|
|
Wadau wakiwa ukumbini.
|
|
Baadhi ya viongozi katik Mtaa wa Mbezi Beach A wakiwa ukumbini
|
|
Baadhi ya viongozi wakiwa ukumbini.
|
|
Amsha-amsha ikiendelea ukumbini baada ya Diwani Mutta kuhutubia.
|
|
Mama John Komba na Diwani Mutaa wakifurahia shughuli.
|
|
Shamra shamra zikaendelea katika kukamilisha hafla hiyo.
|
|
MC wa hafla hiyo Komredi Adimu (T shirt ya njano), akizidi kukoleza Shamra shamra zikaendelea katika kukamilisha hafla hiyo. |
|
Mhudhuriaji mmoja wa hafla hiyo akisaidiwa kuinuka wakati akilia ambapo alisema alimkumbuka Hayati Kaptrni John Komba.
|
|
""Hongera Mwenyekiti, hafla imependeza sana na imekuwa ya manufaa kwa Chama, UVCCM Tawi la Kibomu mmekuwa wa mfano wa kuigwa", Diwani Mutta akimwambia Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Kibomu wakati wakiagana mwishoni mwa hafla hiyo.
| CCM Blog/Bashir Nkoromo
|
|
©Sept. 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇