LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 9, 2025

RAIS DK. SAMIA ANYAKA FOMU INEC KUOMBA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA URAIS

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 9, 2025, amechukua fomu ambayo

amekabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma, kwa ajili ya kuomba kuteuliwa na INEC kugombea urais kwa tiketi ya CCM.


Rais Dk. Samia aliambatana na mgombea mwenza wake, Katibu Mkuu wa CCM Dk. Emmanuel Nchimbi na baadhi ya viongozi na makadana wanchama wa CCM.


Baada ya kuchukua fomu, Rais Samia ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM alizungumza na wanachama wa CCM.


Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Dk. Samia kuwania rasmi kiti cha urais ikiwa ni miaka minne iliyopita, akiwa Makamu wa Rais  aliapishwa kuiongoza Tanzania kufatia kifo cha aliyekuwa Rais wa wakati huo Dk. John Pombe Magufuli.


Rais Dk. Samia aliteuliwa rasmi na na CCM kuwa mgombea wake wa urais  kupitia mkutano mkuu maalum wa kitaifa uliofanyika mwishoni mwa wiki ya Januari 19 2025. 


Mkutano huo ulifa.yika Dodoma, na wajumbe zaidi ya 1,900 walikubali kwa kauli moja kumpotisha Dk. Samia kama mgombea urais na Dk. Emmanuel Nchimbi kama mgombea mwenza (makamu wa rais)

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele katika Ofisi za Tume hiyo Njedengwa Jijini Dodoma leo. Agosti 9, 2025. Kushoto ni Mgombea Mwenza wake Katibu Mkuu wa CCM Dk. Emmanuel Nchimbi.


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages