LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 6, 2021

TPC YAZINDUA DUKA LA POSTA MTANDAONI, YAUNGANA NA MADUKA 670 DUNIANI

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Zainab Chaula (wa pili kushoto) na Kaimu Postamasta Mkuu, Macrice Ndobo (wa pili kulia) wakipiga makofi baada kuzindua  rasmi Duka la Posta Mtandaoni (Posta Online Shop) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani leo Oktoba 6, 2021 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. Kundo amezindua duka hilo kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Ashatu Kijaji.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew  akibofya kitufe cha kompyuta mpakato ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Duka la Posta Mtandaoni.
Kaimu Postamasta Mkuu wa  Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo akielezea jinsi duka hilo la mtandaoni litakavyokuwa linafanya kazi kwa watu kununua na kuuza pamoja na kusafirisha bidhaa duniani. Mapaka sasa watu 423  wamejisajili kwenye duka  hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya watendaji na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa duka la Posta mtandaoni.




Msanii Mrisho Mpoto ambaye ni Balozi wa Posta akighani wakati bendi yake ilipokuwa inatumbuiza wakati wa maadhimisho hayo.
Mhamasishaji bora wananachi kujiunga na duka hilo la Posta Mtandaoni akikabidhiwa tuzo ya cheti na Naibu Waziri, Kundo.

 Naibu Waziri, Kundo akimkabidhi tuzo ya cheti Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Awesome Food, Jesca Alphonce kwa kuwa muuzaji bora wa bidhaa zake kwenye dula la posta mtandaoni. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


KATIKA kuongeza ubunifu wenye tija kwenye masuala ya uchumi na kuondokana na changamoto ya UVICO-19 unaoikabili Dunia,Shirika la Posta Tanzania (TPC) limewataka wafanyabiashara, wajasiriamali wa mtandao pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo kujisajili katika huduma ya duka mtandao (Posta Online shop) lenye zaidi ya lugha 20 zinazotumiwa duniani ili kuongeza wigo wa biashara zao.

Kaimu Posta Masta Mkuu wa TPC,  Macrice Mbodo amesema hayo Jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani yaliyoambatana na uzinduzi rasmi wa duka la Posta mtandaoni  utakaofanikisha mikakati ya shirika hilo kukuza uchumi na kujitegemea huku akisema duka hilo pia limeenzi lugha ya kiswahili.

Amesema kupitia uzinduzi rasmi wa duka hilo,wamekuja na huduma mpya tatu ambazo ni Posta Kiganjani, Vituo vya Huduma kwa wateja Pamoja na Duka Mtandao. 

Mbodo anasema huduma hiyo inategemea zaidi ushirikiano wa watanzania na kwamba  iwapo wizara na taasisi zote zitafungua vituo vya huduma pamoja posta ni wazi huduma nyingi wanazotoa zitapatikana kwa urahisi na kuongeza mapato yatayosaidia kukuza uchumi na kuondoa utegemezi.

"Kupitia huduma ya duka mtandao ambayo inasimamiwa na shirika la Posta Tanzania tumefanikiwa kupata zaidi ya Sh.milioni 300 huku Watanzania wengi wakiendelea kujisajili kutumia huduma hii, juhudi zetu ni kuhakikisha Watanzania wengi wanajiunga na duka mtandao ili kufanya biashara zao kwa gharama ndogo,"anaeleza.

Licha ya hayo Mbodo anasema iwapo Watanzania watatumia shirika hilo ni wazi kuwa thamani ya TPC siku moja itakuwa kama Amazon au Ali Baba kwenye eneo hilo la duka mtandao.

"Tumepiga hatua,kupitia duka mtandao Mteja atajisajili kwa njia ya mtandao, ataweka bidhaa zake na maelezo kama bei, uzito na akishamaliza mteja ataweza kuona bidhaa hizo kupitia duka  mtandao (Posta Online shop)Mteja anaweza kupitia huduma za kifedha za Tigopesa, M-pesa, Airtel Money au kwa Credit Card na Shirika la Posta litaenda kuchukua hiyo bidhaa kwa muuzaji na kuipeleka kwa mteja iwe ndani au nje ya nchi," amesema.

Amesema, kupitia Shirika la Posta, mteja anaweza akanunua bidhaa tofauti kwa wakati mmoja na akalipia hapo hapo alipo na  atapelekewa hadi nyumbani.

Akielezea dhana inayosambaa kuhusiana na utapeli kwa bidhaa za mtandao, Kaimu huyo amesema Shirika la Posta ni la kiserikali ila itakapotokea kuna hitilafu kwenye bidhaa Shirika litamtafuta muuzaji wa bidhaa ili iweze kubadilishwa na kuipeleka tena kwa mteja, Shirika  hili ni kongwe na limeenea nchi nzima.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Habari , Mawasiliano,Teknolojia na Habari Mhandisi Kundo Methew ambaye katika maadhimisho hayo amemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Dkt Ashatu Kijaji  ametumia nafasi hiyo kueleza Umma historia ya Shirika  la Posta Tanzania (TPC)na kueleza kuwa lilianzishwa mwaka 1994, ambapo hadi sasa linatoa huduma nchini kote na kujiunga na mashirika mengine zaidi ya 670  duniani.

"TPC inatoa huduma kupokea na kusambaza barua, vifurushi, kadi, magazeti, majarida, huduma ya mtandao, huduma pamoja na nyingine nyingi,dira ya TPC ni kuhutoa huduma ndani na nje katika ubora, kwa wakati na kueleweka,tutahakikisha tunatoa huduma ya bora ambayo inatambulika ulimwenguni na kukidhi malengo ya wateja,"amesema.

Amesema, mafanikio ya biashara mtandaoni yapo mikononi mwa jamii  kwamba historia inaonesha kuwa shirika hilo katika miaka ya nyuma limeweza kufanya vizuri katika utoaji huduma jambo ambalo limechangia kufika kidigitali zaidi.

"Kupitia mafanikio hayo makubwa ambayo yameonekana katika mashirika mengine duniani TPC imekuja upya ili kuhakikisha linakuwa shirika ambalo litachangia ukuaji wa uchumi nchini kwa kasi,ukijiunga na duka mtandao asilimia 100 biashara yako ipo salama kwani ni huduma ambayo inasimamiwa na shirika letu  wenyewe,” anasema.

Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa huduma hiyo itawezesha wateja kufuatilia barua na vifurushi vyao kujua wapi vimefika kupitia simu zao za mkononi. 

"Lengo na mikakati yetu ni kuhakikisha kuwa shirika  hili linakuwa mchangiaji mkubwa wa uchumi wa nchi kama nchi nyingine duniani zinavyofanya,shirika limejitanua zaidi lina ofisi zaidi ya 350 nchini kote hivyo ni vema taasisi za Serikali, mashirika na sekta binafsi kujiunga na posta ili kupata huduma ya pamoja kwa wakati,ameeleza..

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages