Jun 6, 2021

MKURABITA KURASIMISHA MASHAMBA YA WAKULIMA WA MIWA MKUNDI, WILAYANI KILOSA+video

 



Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), Anthony Temu akielezea umuhimu wa wananchi  wa Kijiji cha Mkundi, Kata ya Dumila, wilayani Kilosa, Morogoro kushiriki kazi ya kupima mashamba yao ya kilimo cha miwa ili wapate hati miliki za kimila.

Temu aliwaeleza kuwa wakipata hati miliki za kimila wataweza kuzitumia kuweka kama dhamana kukopa fedha benki na taasisi zingine za fedha zitakazowasaidia kupanua kilimo cha miwa na kuboresha miradi yao mingine.

Aliyazungumza hayo  katika kikao cha Halmashauri ya Kijiji cha Mkundi na wakati wa Mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kijiji hicho, ambapo waliukubali mpango huo kwa kauli moja na kuishukuru Mkurabita kwa kuwakumbuka na kuuomba uongozi wa Mkurabita kupima pia mashamba mengine zaidi.

Kazi ya upimaji ardhi inayoshirikisha maafisa wa Mkurabita wakiongozwa na Meneja Temu na maafisa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa pamoja na kamati maalumu iliyoundwa na wanakijiji imeanza juzi. 
 


Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Mkundi wakiwa katika kikao na uongozi wa Mkurabita kupanga mikakati ya kufanikisha urasimishaji wa ardhi.
Wajumbe wa Halmahauri ya Kijiji wakiwa meza kuu pamoja na uongozi wa Mkurabita na maafisa wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji.
Sehemu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Viongozi wa Kijiji wakiangali ramani ya Kijiji ch Mkundi katika hati waliyokabidhiwa kutoka wilayani.
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Kijiji ch Mkundi,  Boniventure Flawan  akiwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika kazi ya upimaji wa ardhi.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mkundi, Martine Mshanga akifafanua jambo wakati wa mkutano wa hadhara.

Wananchi wakiuliza maswali



Mdau Nakuomba uendelee kusikiliza clip hii ya video ujue yaliyojiri kwenye mkutano huo wa kijiji....
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM.
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages