Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Komredi Kheri James akisalimiana na Viongozi wa CCM na UVCCM alipopokelewa katika Wilaya ya Mkuranga alipowasili kuanza ziara ya kikazi katika mkoa wa Pwani, jana.
Mkuranga, PWANI
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Komredi Kheri James ameanza ziara ya kikazi Katika mkoa wa Pwani kuhamasisha uhai wa Chama na Jumuiya hiyo.
Komredi Kheri alianza jana ziara hiyo katika Wilaya ya Mkuranga ambako amepokelewa na Viongozi mbalimbali katika wa Chama Cha Mapinduzi na UVCCM mkoa wa Pwani na Wilaya ya Mkuranga.
Akiwa Wilayani Mkuranga Komred kheri James amezungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu na Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM katika wilaya hiyo ya Mkuranga.
Katika mkutano huo Komred Kheri James amewapongeza Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi ambao Chama kimeuoata katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana wa 2020.
Komredi Kheri James katika hotuba yake amesisitiza Viongozi wa Chama na Jumuiya kufanya ziara, vikao na kuweka mikakati ya kuongeza wanachama pamoja na kubuni miradi itakayo wezesha Chama na Jumuiya kuweza kujitegemea katika maeneo yao.
Pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa Chama na Jumuiya kujiandaa kikamilifu kuelekea katika Uchaguzi wa Chama utakao fanyika mwaka 2022.
Amewataka Viongozi wote wa Chama kila mmoja katika eneo lake kuendeleza ushirikiano kwa Viongozi wa Serikali hasa katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya tano inapoendelea kutekeleza ahadi zilizo tolewa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 -2025.
Katika Ziara hiyo Komred Kheri James ameambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Ramadhani Maneno na Kamati ya Utekelezaji Mkoa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa huo Samaha Seif Said.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇