LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 15, 2020

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YAWAPIGA 'MSASA' WATOA HUDUMA YA HABARI MITANDAONI, LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles akizungumza mbele ya   Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni, wakati akifungua Mkutano kati ya Tume hiyo na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni, uliofanyika leo katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.


Dar es Salaam, Tanzania

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutana na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni ‘Online Content Service Providers’ nchini na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuwezesha kutoa huduma bora wakati huu wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ulipangwa kufanyika Siku ya Jumatano ya Oktoba 28, 2020.


Mkutano huo umefanyika leo Jumanne Septemba 15,2020 katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es salaam .


Akifungua Mkutano huo katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere, leo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa Uchaguzi Dk. Wilson Charles amesema Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni ni wadau muhimu katika mchakato wa uchaguzi ndiyo maana NEC imeamua kukutana nao ili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya uchaguzi ili waweze kuandika habari kwa usahihi na kwa kujali maslahi ya nchi ikiwemo kulinda amani ya nchi.


“Tume ya Taifa ya Uchaguzi tunavipongeza vyombo vya habari mtandaoni kwa ushirikiano ambao mmekuwa mkitupatia. Tumewaita ili kuwajengea uelewa kuhusu mkachato wa uchaguzi,tunaamini kuwa mna nafasi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu taratibu mbalimbali za uchaguzi”,amesema Dkt. Charles.


Aidha aliwataka waandishi wa habari kuvipa nafasi sawa vyama vyote vya siasa na kuepuka kuandika habari zenye kuhamasisha vurugu na kusababisha uvunjivu wa amani.


“Kipindi cha Kampeni za uchaguzi huwa kuna joto la uchaguzi ambapo joto la kuvunja amani nalo huongezeka. Naomba tulinde amani ya nchi yetu kwa kuepuka kuandika habari zenye kuleta chuki”,amesema.


Katika hatua nyingine alivitaka vyama vya siasa kufuata maadili ya uchaguzi na sheria za nchi na kuhakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu huku akivikumbusha vyombo vya habari kuepuka kuandika kauli na matamshi ya kuvunja amani.


“Kuanzia sasa tutachukua hatua kali kwa viongozi wanaotoa matamshi ya kuvunja amani. Hata wewe mwandishi wa habari ukiandika habari zenye kuunga mkono matamshi hayo nawe utakuwa unavunja amani”,ameongeza Dkt. Charles.


Mkurugenzi huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ametumia fursa hiyo kuviomba vyombo vya habari kuelimisha jamii kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza sera za wagombea na kupiga kura Oktoba 28,2020 ili kupata viongozi wanaowataka watakaowaletea maendeleo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu kwa Mpigakura, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Giveness Aswile akitoa ufafanuzi kuhusu elimu ya mpigakura katika Mkutano wa NEC na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (Online Content Service Providers) uliofanyika leo katika Ukumbu wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa lengo la NEC kupanua uelewa kwa watoa huduma hao katika kuhabarisha umma kwa weledi katika habari za kamapeni, Uchaguzi na matokeo yake, katika mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Jumatano, Oktoba 28, mwaka huu. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Habari na Mawasiliano kwa Umma,  ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) akizungumzia masuala ya kisheria kuhusu kuripoti masuala ya Uchaguzi katika Mkutano wa NEC na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni (Online Content Service Providers) uliofanyika leo katika Ukumbu wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa lengo la NEC kupanua uelewa kwa watoa huduma hao katika kuhabarisha umma kwa weledi katika habari za kamapeni, Uchaguzi na matokeo yake, katika mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Jumatano, Oktoba 28, mwaka huu. 

👇👇Baadhi ya Washiriki kwenye mkutano huo








No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages