Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma kimepitisha Azimio la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu kwa kuelekeza zaidi ya Shilingi Tril.11.5 mkoani Kigoma kwa ajili ya kutekeleza miradi inayoenldelea kuleta mabadiliko makubwa katika Sekta za kutolea huduma za Jamii pamoja na kuuufanya mkoa kuwa kitovu cha Uchumi kwa Ukanda wa Magharibi.
Sambamba na pongezi hizo zilizotolewa kupitia Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM Mkoa kwa ajili ya kupokea Taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2024, Chama kimetoa hati ya pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Akizungumza kabla ya kufunga kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mhe. Jamal Tamim amesema pongezi hizo ni matokeo ya hali halisi ya kazi nzuri zinazoonekana wazi za utekelezaji wa miradi na uthabiti katika usimamizi unaofanywa na watendaji wa serikali.
Katika hatua nyingine Tamim amewataka viongozi wa Serikali na wale wa chama kutumia muda mwingi katika kusikiliza shida za wananchi na kuwasaidia kutatua kero zao.
Amesema viongozi wa chama wanajukumu kubwa la kuendelea kuwaeleza wananchi kuhusu kazi nzuri zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita ambazo zimelenga kuleta mapinduzi ya kimaendeleo na kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Tamim amewakumbusha wabunge na Madiwani kuendelea kuwa karibu na wananchi, kushiriki shughuli za maendeleo pamoja na vikao ili wawe sehemu yao badala ya kurejea katika maeneo yao ya kiutawala zinapokaribia nyakati za uchaguzi.
Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa, ametoa wito kwa jamii kuepuka vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto huku akisisitiza wakazi kutosita kutoa taarifa au ushahidi kwenye kesi zinazohusiana na matukio hayo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mhe. Jamal Tamim akikabidhi hati ya pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
RC Andengenye akitoa shukrani kwa uongozi huo wa CCM Mkoa kwa kutambua jitihada za Rais Samia na Serikali kwa ujumla.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Jamal Tamim akitoa pongezi hizo kwa Rais Samia.
Makada wa CCM wakiwa katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇