Katika kipindi cha miaka minne Taasisi ya MOI imefanikiwa kuanzisha huduma zaidi ya 10 za kibobezi ambazo hapo awali ziliwalazimu wagonjwa kuzifuata nje ya nchi. Huduma zilizoanzishwa ni pamoja na:
1. Upasuaji na uchunguzi wa ubongo bila kufungua fuvu ambapo hadi sasa wagonjwa 62 wamehudumiwa.
2. Upasuaji wa Nyonga na magoti wa marudio wagonjwa 74 Wamehudumiwa
3. Upasuaji wa mgongo kwa njia ya matundu wagonjwa 17 wamefanyiwa
4. Matibabu ya kiharusi kwa kupitia mishipa mikubwa ya damu ya paja wagonjwa 41 wamehudumiwa
5. Upasuaji wa kunyoosha mgongo uliopinda (Kibiongo) wagonjwa 64 wamehudumiwa.
6. Kuondoa uvimbe kwenye ubongo kupitia tundu la pua , wagonjwa 41 wamehudumiwa
7. Huduma ya maumivu sugu ya mgongo, wagonjwa 607 Wamehudumiwa
8. Huduma ya wagonjwa maalum na wagonjwa wa kimataifa, wagonjwa 6,106 wamehudumiwa.
9. Huduma ya mkono wa umeme ambapo mpaka sasa wagonjwa 6 wamewekewa mkono bandia. 10. kutengeneza viungo bandia kwa teknolojia ya ‘3D’ kwa wagonjwa wanne (4).
Pia, Taasisi ya MOI imeendelea kutoa huduma nyingine za kibingwa Bobezi na kupunguza rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi kama ifuatavyo:
1. Upandikizaji wa nyonga bandia wagonjwa 728 wamehudumiwa
2. Upandikizaji wa goti bandia wagonjwa 636 wamehudumiwa
3. Upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu wagonjwa 1,115 wamehudumiwa
4. Upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo (Aneurysm) 14 wamehudumiwa
5. Upasuaji wa mfupa wa kiuno wagonjwa 395 wamehudumiwa
6. Upasuaji wa kichwa kikubwa na mgongo wazi watoto 1,797 wamehudumiwa
7. Upasuaji wa ubongo kwa kufungua fuvu 815
Upasuaji wa mgongo kwa njia ya matundu wagonjwa 17 wamefanyiwa
4. Matibabu ya kiharusi kwa kupitia mishipa mikubwa ya damu ya paja wagonjwa 41 wamehudumiwa
5. Upasuaji wa kunyoosha mgongo uliopinda (Kibiongo) wagonjwa 64 wamehudumiwa.
6. Kuondoa uvimbe kwenye ubongo kupitia tundu la pua , wagonjwa 41 wamehudumiwa
7. Huduma ya maumivu sugu ya mgongo, wagonjwa 607 Wamehudumiwa
8. Huduma ya wagonjwa maalum na wagonjwa wa kimataifa, wagonjwa 6,106 wamehudumiwa.
9. Huduma ya mkono wa umeme ambapo mpaka sasa wagonjwa 6 wamewekewa mkono bandia. 10. kutengeneza viungo bandia kwa teknolojia ya ‘3D’ kwa wagonjwa wanne (4).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Mhe. Balozi, Dkt. Mpoki Ulisubisiya, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita tarehe 5 Machi, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.2.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇