Mar 6, 2025

HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO YAANZA MUHIMBILI

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Imeanzisha matibabu ya kuziba mapengo  Vipandikizi Meno (Dental Implant), ambapo mzizi bandia hupandikizwa kwenye taya, kisha kuwekewa meno juu yake yanayogandishwa na kutumika kama sehemu ya meno yake ya kuzaliwa nayo.


Aidha, Serikali imewezesha hospitali hiyo kununua mashine ya kisasa kabisa inayowezesha uchunguzi wa magonjwa ya mifupa ya taya pamoja na CT scan ya uso na kichwa kusaidia kupanga upandikizaji wa vipandikizi vya meno ambapo tangu kununuliwa mwishoni mwa mwaka 2024 tayari wagonjwa 2,251 wamenufaika.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma ya Upasuaji wa hospitali hiyo, Dkt. Rachel Mhaville alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Machi 6, 2025, kuhusu mafanikio ya MNH katika miaka minne ya ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Dkt. Mhaville ambaye kwenye mkutano huo alikuwa anazungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa MNH, Prof. Mohamed Janabi, amesema kuwa wameanzisha huduma nyingine ya kuondoa sehemu yenye ugonjwa kwenye taya kisha kuvuna sehemu ya mbavu pamoja na mfupa wa nyonga kwa kutumia vipandikizi maalum kuunda mfupa wa taya jipya la chini ili kumrejeshea mgonjwa muonekano mzuri lakini pia huweza kupandikizwa meno na kumrejeshea mgonjwa uwezo wa kula tena.


Dkt. Mhavile akizungumza katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.


Mkurugenzi Msaidiz wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa akitoa neno la kuhitimisha mkutano huo.


.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages