LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 7, 2020

OKASH: JESHI KUBWA LA WANAWAKE TUTAMFANYIA KAMPENI DK MAGUFULI NYUMBA KWA NYUMBA, KITANDA KWA KITANDA



Mgombea Ubynge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Halima Okash akipokea Kitabu cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za CCM jijini Dodoma hivi karibuni. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Na Richard Mwaikenda, Dodoma

LICHA ya kuwa siku ya kusikiliza sera, ilani na mikakati yay a ushindi, pia ilikuwa ni siku ya watu kuburudika, kufurahi, kucheka kutokana na vionjo mbalimbali vilivyokuwepo siku ya uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM),  kwenye Uwanja wa Jamhuri  jijini Dodoma wiki moja iliyopita.

Mgombea Ubunge Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Halima Okash alikuwa ni miongoni mwa wagombea ubunge waliobahatika kupanda jukwaa kuu ambapo aliwachekesha viongozi waliokuwepo jukwaani wakiongozwa na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli.

Waheshimiwa viongozi waliokuwepo waliangua vicheko pale Okash alipoieleza kadamnasi iliyofurika uwanjani hapo kuwa atahakikisha yeye na akina mama wenzie  ambao ni jeshi kubwa wanamfanyia kampeni za nguvu  kwa kwenda nyumba kwa nyuma,  chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda, godoro kwa godoro hadi wahakikishe ushindi mkubwa kwa Dk. Magufuli ambaye ameifanyia makubwa Nchikwamuda mfupiwa miaka mitano.

“Naahidi kuwa kura zote za ushindi tunampatia akina mama  maana ni Jeshi Kubwa na kwamba tutakwenda kuzisaka nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda, godoro kwa godoro mpaka tuhakikishe ushindi unakwenda kwa Dk. Magufuli,”alisema Okash huku akisababisha viongozi na wananchi kuangua kicheko.

Baada ya kumaliza kutoa vionjo hivyo vya kumnadi Dk. Magufuli alikwenda kukabidhiwa Kitabu cha Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ali na kuelekea kukaa sehemu aliyopangiwa, huku akiacha gumzo.

Okash akipita mbele ya viongozi; Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk.John Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Dk. Jakaya Kikwete.
Okash akimnadi Dk. Magufuli





 Okash akiondoka jukwaakuubaadaya kufanyakazi ya kumnadi Dk. Magufuli na wagombea wengine wa CCM

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages