Apr 28, 2025

JK ASHIRIKI KUWANOA KATIKA CHUO KIKUU CHA HARVARD, MAREKANI, MAWAZIRI WA FEDHA NA WA MIPANGO WA NCHI ZINAZOENDELEA

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete yuko mjini Boston, Marekani, ambako anashiriki kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha na Mawaziri wa Mipango kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea.

Mafunzo hayo yanafanyika chini ya Mpango wa Uongozi wa Ngazi ya Mawaziri wa Harvard, maarufu kama Harvard Ministerial Leadership Program, unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard.

Dk. Kikwete ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu walioalikwa kushiriki kama wakufunzi, wakitumia uzoefu wao wa uongozi kuhamasisha na kuwajengea uwezo viongozi wa kizazi kipya.

Mbali na Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu, mafunzo haya pia yanashirikisha Wakuu wa Taasisi za Kimataifa, wawakilishi wa mashirika binafsi, pamoja na mabingwa wa masuala ya sera, uchumi na maendeleo kutoka maeneo mbalimbali duniani.







 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages