LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 18, 2020

JPM APIGA SIMU, AAMURU ASKARI WA SUMA JKT WANAOPIGISHA VICHURACHURA WANANCHI STENDI MPYA YA DODOMA WAONDOLEWE MARA MOJA

 “Suma JKT wanafanya kazi nzuri hawajaanzia stendi ya Dodoma, wapo pale Feri DSM, Mwanza hatujaona Watu wakipigishwa vichurachura, wanaofanya hivyo waondolewe mara moja, wabaki maaskari wanaowahudumia watu, sitaki watu wangu warushwe vichura kwenye nchi ya amani”-JPM Live kwa Simu
Wananchi wakiingia na wengine kutoka katika Stendi mpya ya Kisasa ya Dodoma.


RAIS Dk.John Magufuli ametoa maelekezo kadhaa kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuhusu Stendi Kuu ya mabasi ya jijini humo yakiwemo ya kuhakikisha wajasiriamali wadogo,Mama Lishe, waendesha bodaboda na daladala kufika kituoni hapo bila kusumbuliwa.

Pia ametoa maelekezo ya askari wa Suma JKT wenye tabia ya kupigisha watu vichura kuacha mara moja, kwani hayuko tayari kuona Watanzania waliohuru kwenye nchi wakirushwa vichura na ametumia nafasi hiyo kumwambia Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuacha Suma JKT wanaohudumia watu na sio wanaotesa watu.

Akizungumza leo Juni 18, 2020 kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Rais Magufuli alianza kueleza "Nakupongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa ubunifu na uchapakazi katika kuleta maendeleo, katika jiji letu jipya ambalo ni Dodoma, Jiji ambalo ni makao makuu ya nchi

"Lakini nawapongeza wadau wa stendi hiyo ambao jana walikuwa wanazungumza pointi nyingi ambazo mimi nimekubaliana nazo, moja ya pointi ambayo niliiipenda na nakubaliana nao ni hili la kuruhusu watu wetu wa kufanyabiashara ndogondogo kushiriki kufanya biashara hapo , hakuna sababu ya kuwa namna stendi ya Watanzania wote , wa maisha yote halafu hao hawashiriki hata kuuza zabibu hapo, tutaitangazaje stendi.

"Mtu anatoka kijijini kule, watani zangu Wagogo ametoka kule amekuja kwenye basi halafu anateremka pale unamlazimisha akale chakula cha shilingi 5000 , kwa hiyo mama lishe lazima wawepo kwa ajili ya kuuza chakula cha shilingi 500 badala ya shilingi 5000.Haya ndio maisha yetu Watanzania lakini ieleweke hiyo stendi haikujengwa kwa ajili ya watu matajiri, stendi nimeijenga kwa ajili ya watu wote wakiwemo masikini,"amesema Dk.Magufuli.

Ameongeza kuwa kwa hiyo kinapofanyika kitu cha maendeleo katika nchi ya Tanzania haiwezekani tukajenga maisha kwa ajili ya watu fulani tu na hicho ndicho akipendi,

"Watanzania wote wa maisha yote wa levo zote washiriki kujitafutia riziki katika maeneo hayo , ,kwa hiyo nitafurahi siku moja mtu anayeuza juisi ,karanga, anampa mtu aliyekuwa kwenye basi,lakini kuteremka kila mmoja utaenda kuzinunua zabibu za kwenye hoteli, ya shilingi 6000.

"Kwa hao vijana nimekubaliana nao wamezungumza pointi nzuri sana .Lakini nimekubaliana nao kuhusu suala la daladala ,haiwezekani kwenye daladala watu wateremke halafu waanze kutembea ,nilazima Jiji litengeneze mazingira watu wa daladala waweze kufika pale , wabodaboda waweze kufika,wa bajaji waweze kufika , ili kusudi hata mvua ikiwa inanyesha mtu asiweze kutembea na mizigo yake.

"Waapo wengine wanateremshwa pale wagonjwa wanaenda hospitalini sasa anaanza tena kutembea kwenda kushika daladala ,kwa hiyo mtengeneze mazingira ya kuhakikisha daladala zinaweza kuwa na eneo lao pale,zifike ziteremshe watu na kisha wanaendelea na hiyo ndio connection au kama mishipa katika mwili wa binadamu inavyofanya kazi,"amesema Rais Magufuli.

Ameongeza kwamba "Na hiyo ndio connection ya maendeleo ya Jiji la Dodoma,lakini pia lingine ambalo nimekubaliana nalo ni kwa Suma JKT kuwapigisha vyura, hapo sio jeshini , hapo Suma JKT mmewaajiri kwa ajili ya kulinda usalama wa raia wa Tanzania ,hawakuajiriwa hapo kuwapigisha vichura, na bahati nzuri Suma JKT wanafanya kazi nzuri ,hawajaanzia stendi ya Dodoma.

"Pale feri ya Dar es Salaam kuna suma JKT hatujaona watu wakirushwa na kupigishwa kichura pale,feri Kigamboni, pale feri Mwanza kuna Suma JKT hawapigishi watu vichura, sasa ndio nasema wewe ambao umeingia nao mkataba nina uhakika haukusema mtu akikosea arushwe kichura.

"Kwa hiyo kama wanaendelea kuwarusha kichura basi hao wanaowarusha wananchi kichura watolewe, wabaki maaskari wa JKT wanaowahudumiwa watu,sio kurusha kichura, sitaki kuona watu wangu wanarushwa kichura kwenye nchi iliyohuru,tulipata uhuru ,kwa hiyo mimi nimekubaliana nayo,amesema.

Haha Hi yo ambalo Rais Magufuli hakubaliani nalo ni kuuweka wapiga debe."Wapiga debe ndio wakati nwingine wanageuka kuwa majizi na kurubuni watu, wale hapana, kwenda pale na kuanza kupiga debe sio kitu kizuri ,kwanini mtu apige debe,akapige debe la nyumbani kwake.Kupiga debe pale hiyo sio njia ajira nzuri,ajira nzuri ni watu kwenda kufanyabiashara kwa kuuza zabibu,karanga huo ndio ujasiriamali.

"Lakini utengeneze utaratibu wale wenye vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo nao watengenezewe maeneo ya kufanyabiashara ,lazima wafanye biashara kwa watu,nashukuru Mkurugenzi umeenda kuzungumza nao ,hiyo inaonesha na wewe ni kijana mzuri unayependa maendeleo kwa ajili ya Jiji la Dodoma."

Kwa upande wakeMkurugenz wa Jiji Kunambi amesema amepokea maelekezo yote na anakwenda kuyafanyia kazi kwa haraka sana.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages