LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 7, 2025

RAIS SAMIA AWASILI NCHINI ANGOLA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  4 De Fevereiro Luanda kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola tarehe 07 Aprili, 2025. Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Angola Mhe. JoĂŁo Manuel Gonçalves Lourenço na lengo la Ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha zaidi mahusiano ya kihistoria na kidugu baina ya Tanzania na Angola.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola  Mhe. TĂ©te AntĂłnio mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 De Fevereiro Luanda kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola tarehe 07 Aprili, 2025.










 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages