Mbunge Dk. Ritha Kabati
Na Richard
Mwaikenda
MBUNGE wa
Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Dk. Ritha Kabati amechapisha kitabu cha kurasa 15
kinachoelezea alivyoshiriki katika kampeni
ya kuelimisha wananchi jinsi ya kukabiliana na janga la Corona.
Kampeni hiyo
ameifanya katika vijiji mbalimbali vilivyopo katika wilaya tatu za mkoa wa
Iringa, ambazo ni Mufindi, Kilolo na Iringa.
Katika
kuhakikisha Serikali inafanikisha azma yake ya kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid19 unaotokana na virusi vya Corona,
ulioenea Duniani kote. Dk. Kabati, ameamua kufanya ziara ya mkoa mzima ili kufikisha ujumbe wa
namna bora ya kujihadhari na usambazaji wa ugonjwa huo.
Alianza
ziara yake katika Wilaya ya Iringa Vijijini, ambapo alitoa elimu ya nyumba kwa
nyumba kuona namna wanavyochukua tahadhari na wanavyoutafsiri ugonjwa huo.
Aliweza kuzifikia kata zote za wilaya hiyo na kuonana na wananchi pamoja na
viongozi wa serikali, CCM, UWT na Jumuia zake zote.
Katika
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, Dk. Kabati, alitembelea pia Kituo
cha Afya cha Ipamba ili kujua utayari
wao wa kugundua watu kwenye
kuhisiwa kupata maambukizi ya ugonjwa
huo hatari.
Katika Kituo
hicho, Dk. Kabati alibaini uwepo wa utaratibu maalumu wa kuwapima joto watu
wote wanaoingia hapo kwa kuwa na kifaa
maalumu cha kupimia joto. Uwepo wa
chumba maalumu kilichotengwa kwa watakaohisiwa.
Wameagiza vifaa maalumu kwa ajili ya wauguzi kujikinga wakati wa
kutoa tiba. Utoaji elimu kuhusu Corona ulikuwa unaendelea.
Katika
Wilaya ya Kilolo, Mbunge huyo ambaye ni mfano wa kuigwa kwa uchapakazi,
alijikita kutembelea katika maeneo ya biashara na yenye mikusanyiko ya watu,
ambapo alibaini baadhi ya maeneo wakiwa wamechukua tahadhari kwa kuweka maji tiririka
na vitakasa mikono. Maneo hayo ni:Kata ya Ilula, Nyalumbu, Ruaha Mbuyuni,
Lugalo na Mtitu.
Pia,
aliyabaini maeneo yanayohitaji kutolewa elimu zaidi ambayo ni: Kata ya Kimara,
Idete, Nga’ng’ange, Dabaga na nyinginezo kutoka Kilolo Milimani. Pia alishauri
elimu itolewe zaidi katika maeneo ya usafiri wa Daladala, Bodaboda na Bajaji
ikiwa na uwekaji wa maji tiririka na vitakasa mikono.
Alizungumza na
viongozi mbalimbali wakiwemo wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), juu ya
kuendelea kutoa elimu na kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii inayowazunguka, ambapo
pia aliwawezesha kiasi cha fedha ili kununua vifaa vya kujikinga na maambukizi
ya Corona.
Katika
Wilaya ya Iringa Mjini, Dk. Kabati, alianza kwa kuitembelea Hospitali ya Mkoa wa Iringa, ambapo
alisikitishwa kuona kutokuwepo utayari
wa vipima joto vya kuwatambua wanaohisiwa kuwa na Corona, jambo ambalo ni
hatari hasa kwa hospitali hiyo inayohudumia watu wengi.
Pia, Dk.
Kabati alipata wasaa wa kutembelea Bohari ya Madawa ya Mkoa wa Iringa na Nyanda
za Juu Kusini kuona upatikanaji wa vifaa
vya Corona, ambapo alibaini ukosefu wa
vifaa muhimu katika kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo hatari.
Katika
Wilaya ya Mufindi, Mbunge huyo alijikita kutembelea maeneo ya biashara na vituo
vya afya kuona namna wanavyochukua tahadhari ya ugonjwa huo, ambapo katika
Mnada wa Kata ya Maduma, alibaini asilimia ya wananchi waliokuwepo, kutokuwa na
wasiwasi wa ugongwa huo licha ya kuwa na elimu kiasi ya kuwepo ugonjwa huo wa
Covid 19 nchini.
Viongozi wa
Kata hiyo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliozungumza nao juu ya suala hilo,
waliahidi kushiriki kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo licha kuwa na changamoto
zifuatazo: Ukosefu wa vifaa vya kujikinga, uhitaji wa watalaamu zaidi wa kutoa
elimu, na uhitaji wa viongozi wa juu wa serikali wanaoweza kupita katika maeneo
ya kutoa elimu.
Alifanya
ziara katika Kituo cha Afya cha Ifwagi kinachohudumia kata nyingi tofauti na
uwezo wake. Ambapo hata hivyo alikuta tayari wameshaweka maji tiririka na vitakasa
mikono, kimeendelea kuwatumia watalaamu wake kutoa elimu juu ya ugonjwa huo,
kimetenga chumba maalumu cha kuwatenga wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na virusi vya
Corona.
Amezitaja
baadhi ya changamoto alizozikuta kituoni hapo kuwa ni; Chumba cha kuwatenga
wagongwa ni kidogo na kina kitanda kimoja,
Kituo hakina vifaa vya kujikinga kwa wauguzi, ikiwemo barakoa, nguo maalumu za
kujikinga na maambukizi, vipimo vya kutambua joto kwa haraka bila ya kugusana,
pia kituo hakina vipeperushi kwa ajili ya kutoa elimu zaidi ya ugonjwa.
Dk. Kabati
amezitaja baadhi ya changamoto alizozibaini kwa ujumla wakati wa ziara zake
kuwa ni; Kutokuwepo kwa vitakasa mikono katika maeneo mengi, bado kuna maeneo
yenye mikusanyiko isiyo ya lazima, baadhi ya watu hawana elimu ya kujikinga dhidi ya corona, bado wapo wakazi wa
maeneo wenye imani potofu kuwa ugonjwa huo hautaweza kusambaa vijijini, vituo
vingi vya afya havina vifaa vya wauguzi
kujikinga na maambukizi ya Corona.
Baada ya
kuona changamoto hizo, Mbunge huyo alichukua hatua za kuwashauri viongozi wa Kata husika kutoa elimu kwa
wananchi juu ya kukabiliana na ugonjwa huo, aliwashauri watalaamu wa afya kuta
elimu ya kitalaamu ili kuondokana na dhana potofu zinazosambazwa mitaani.
Pia,
aliwashauri Watendaji wa Serikali
kufunga biashara za wafanyabiashara
wasiochukua tahadhari ya maambukizi ya Corona, aliagiza vifaa katika
Bohari ya Dawa Mkoa wa Iringa ili kupatiwa wauguzi wa Kituo cha Afya Ifwagi kwa
ajili ya kujilinda. Alikabidhi fedha kwa
viongozi wa kata alizozitembelea kwa ajili ya kununulia vifaa kinga.
Ili kuepukana
na maambukizi ya Corona, Dk. Kabati amewataka wananchi kuepuka kuingia kwenye
misongamano, kukaa umbali wa mita moja na mtu mwingine, kunawa maji tiririka
kwa sabuni pamoja na kutumia vitakasa mikono, usiguse macho,pua na midomo kama
hujanawa, kuvaa barakoa, epuka kuwa karibu sana na mgonjwa, safisa mara kwa
mara vitu unavyovigusa kama vile vikombe, meza, dawati pamoja na simu yako.
Amemalizia
kwa kutoa ushauri kwa Serikali za Vijiji kuchukua hatua dhidi ya
wafanyabiashara na wakazi wasiochukua
hatua za kujihadhari na maambukizi ya
maeneo ya vituo
vya usafiri kama vile, mabasi, daladala, bodaboda na bajaji yawe na maji ya
kunawa pamoja na vitakasa mikono. Masoko na minada isiyochukua tahadhari ya
maambukizi ya Corona yatizamwe upya namna ya utoaji bora wa huduma na viongozi
wa Dini wapatiwe vipeperushi ili kutoa elimu zaidi kwa waumini wao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇