MWENYE njaa usimpe samaki mpe ndoano ili aweze kuvua samaki wengine ili akila apate nguvu na kwenda kuvua samaki wengi zaidi.
Kauli hiyo ameitoa Katibu Mkuu Sayansi wa wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt.James Mdoe wakati akifunga mafunzo ya washindi wa shindano la kitaifa la Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa sio utaratiu wa serikali kugawa fedha kwa wabunifu bali serikali inajukumu la kuwajengea uwezo ili waweze kumiliki bunifu zao kisheria ili mtu mwinvgine asije kujitokeza kufanya kitu alicho kibuni mtu mwingine.
Dkt. Mdoe amesema kuwa wabunifu wengi kuwaendeleza haina maana kuwa tuwape pesa, ni kitendo cha kuwajengea uwezo ili waweze kuendeleza ubunifu ule kwani ni wa mbunifu mwenyewe.
"Sasa jukumu letu kam serikali ni kuwezesha ili uweze kutoka hatua moja kwenda nafasi bora zaidi ili uunifu ule uweze kusaidia zaidi" Amesem Dkt. Mdoe.
Amesema kuwa kunavitu amavyo mbunifu anahitaji ili aweze kuendeleza ubunifu wake na kuwe na mwekezaji ambaye atachukuwa ubunifu wa mbunifu na kufanya kuwa kitu kikubwa na kuwekeza ili biashara iweze kufanyika.
MAfunzo hayo kwa wabunifu wa shindano la MAKSATU yametolewa na Baraza la uwezeshaji uchumi taifa la Sayansi na Teknolojia, Brela, SIDO, TBS na Cosota ambayo yalitolewa kwa siku nnne kwajili ya kuwajengea uwezo na kuonesha fursa mbalimali zilizopo.
Amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha miongozo ya kibunifu, maombi mbalimbali ya ubunifu, ili tuweze kupata wabunifu wengi zaidi kwaajili ya manufaa ya nchi ya sasa na ya baadae.
Kwa upande wa wabunifu, Halima Mpita, amesema kuwa yale yote yaliyoanzishwa na wabunifu lazima yatekelezeke kwaaajili ya kuisaidia jamii yetu, katika mahali wanapoelekea wabunifu hao.
"Safari yetu ya MAKSATU ilianzia aada ya serikali kupitia wizara ya elimu kuundua vipaji 337 na katika kupitia hilo ziliunganishwa na DSI, VETA, COSTECH, DIT,wote hawa walifanya kazi ya pamoja katika kutafuta wabunifu hawa na hatimaye kukawa na mashindano ambayo yalianza machi mwaka huu ndiyo yaliyotupelekea kuwepo hapa leo". Amsema Halima.
Katibu Mkuu Sayansi wa wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia,Dkt.James Mdoe akizungumza na washindi wa shindano la kitaifa la ubunifu wa Sayansi na Teknolojia (2019) (MAKSATU) jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa wabunifu hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH)Dkt. Amos Nungu akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa washindi wa shindano la kitaifa la ubunifu wa Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam leo.
Mbunifu wa mkaa mbadala, Halima Mpita Akizungumza kwa niaba ya wabunifu wengine na kutoa shukurani kwa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufunga mafunzo kwa wabunifu walioshinda katika shindano la kitaifa la Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia
Baadhi ya wabunifu wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu Mkuu Sayansi wa wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia,Dkt.James Mdoe wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa waunifu wa shindano la MAKSATU jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇