Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WADAU
wa kutetea ukatili wa kijinsia wamesema kuwa rushwa ya ngono kwa
wanawake waliofanyiwa lazima wapaze sauti zao ili kukomesha tabia hiyo
katika kujenga utu kwa mwanamke.
Wakizungumza
katika kongamano la maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa
Kijinsia wamesema kuwa wanawake wanaofanyiwa ukatili wa rushwa ya ngono
wamekuwa wakibaki na maumivu huku wengine wakiendelea kuumizwa na rushwa
hiyo.
Kongamano
hilo limeandaliwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao ni Chama
cha Waandishi Habari Wanawake (TAMWA) , Mfuko wa Uhifadhi wa Wanawake ,
Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (Takukuru)pamoja na Jeshi la
Polisi.
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Uhifadhi wa Wanawake Mary Rusimbe amesema rushwa ya ngono
inarudisha nyuma maendeleo ya wanawake kutokana na baadhi ya wanaume
kuhitaji rushwa ya ngono ili kuwawezesha.
Amesema
wameanzisha mtandao wa pamoja wa kupaza sauti za kupinga rushwa za
ngono katika jamii ikiwa ni Wanawake kuzungumza mara anapoona ili
kufanikisha jambo lake lazima atoe rushwa hiyo basi atoe taarifa katika
vyombo husika kwa ajili ya kukomesha.
Amesema
kuwa rushwa iko katika hata shule za msingi ,Sekondari ambapo hao
wanafanyiwa na kisha wanakaa kimya hali ambayo inawafanya kubaki na
majeraha.Rusimbe amesema kuwa kujenga tabia ya jamii kuacha kufumbia macho suala la rushwa ya ngono.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia ni Kataa Rushwa ya Ngono ,Jenga Kizazi chenye usawa.
Mkurugenzi
huyo amesema baadhi yao wanatumia madaraka vibaya sehemu mbalimbali kwa
wanawake na wanaume kuwapandisha vyeo watu kwa ajili ya rushwa hali
ambayo inaondoa utu wa kupanda kwa vyeo hivyo.
Mwakilishi
wa Ubalozi wa Canada Pamela O' Donnell amesema kuwa rushwa ya ngono ipo
duniani kote hivyo mapambano hayo ni ya dunia nzima katika kupaza
sauti.
Nae
Mwakilishi wa Shirika wa Kimataifa linaloshughukia wanawake Agnes Hanti
amesema kuwa mapambano yaendelee katika kujenga utu wa watu katika
kuondokana na rushwa ya ngono.Mwnyekiti
wa Kamati ya Wanawake wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)
Rehema Ludanga amesema kuwa kwa wafanyakazi wanaofanyiwa kutoa taarifa
na hatua zikachukuliwa.
Mratibu
wa Dawati la Jinsia na watoto wa Mkoa wa Kipolisi Ilala Christina
Onyango akizungumza kuhusiana namna jeshi la polisi linavyokabiliana na
rushwa ya ngono
Mwakilishi
wa Shirika la Kimataifa linaloshughukia wanawake Agnes Hanti akitoa
namna Shirika hilo linavyoshirikiana n wadau katika kupinga ukatili wa
kijinsia na rushwa ya ngono.
Wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono wakifatilia mada katika kongamano lililofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇