Mjumbe
maalum na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Prof. Palamagamba John Kabudi amewasilisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenda kwa Rais wa Jamhuri
ya Kenya Mhe Uhuru Kenyatta juu ya masuala mbalimbali ya mashirikiano
baina ya Nchi hizo mbili na Kimataifa.
Katika
Ujumbe huo Tanzania imesema itaiunga mkono Kenya katika nafasi ya Kiti
na Mjumbe asiyewakudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa
kipindi cha mwaka 2021/2022.
Mara
baada ya kukabidhi na kueleza ujumbe wa Rais Dkt Magufuli kwa Rais wa
Kenya Uhuru Kenyata,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepata fursa ya kushiriki
katika uzinduzi wa ripoti ya Mpango wa kujenga umoja na mshikamano baina
ya wakenya ujulikanao kama Building Bridge Initiative,ambapo amewataka
wakenya kushikamana na kuziba mianya ya siasa za kikabila ili kuwa na
Taifa moja kwa ajili ya maendeleo.
Rais
wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa upande wake amesema Taifa hilo kwa
miaka mingi limekuwa likiendeshwa wa siasa za kikabila jambo ambalo
amesema halileti afya kwa ustawi wa Kenya kutokana na kuwa kila baada ya
uchaguzi Taifa hilo huanza kutibu majeraha yaliyotokana na uchaguzi
badala ya kuzingatia masuala ya maendeleo.
Rais
Kenyatta amewataka wanasiasa wenzake kuacha siasa zinazochochea
mgawanyiko na kuwataka kutumia fursa iliyojitokeza kupitia Building
Bridge initiative kutoa maoni ya namna bora ya kufanya siasa za
kistaarabu zisizochochea uhasama.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇