MKUU
wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yonna Mark akizungumza wakati akifungua
mkutano wafanyabiashara eneo la Horohoro wilayani Mkinga ulioandaliwa
na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga ikiwa ni kutoa elimu
juu ya umuhimu wa wao kulipa kodi kwa hiari kulia ni Afisa Mfawidhi wa
Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani na Afisa Habari wa Jumuiya ya
wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria kushoto ni Meneja wa
TRA wilaya za Muheza na MkingaDaudi Njohole
Meneja
wa TRA wilaya za Muheza na MkingaDaudi Njohole akizungumza wakati wa
mkutano huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark akifuatiliwa na
Afisa Mfawidhi Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani na Afisa Habari
wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria
Afisa
Mfawidhi wa Forodha wa TRA Horohoro Bakari Athmani akizungumza kulia ni
Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine
Kiria kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Mark
Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT) Selestine Kiria akieleza jambo katika mkutano huo
Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa kwenye mkutano huo
MKUU
wa wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Yona Mark amewaonya wenyeviti wapya wa
vijiji na vitongoji wilayani humo kuacha kujshughulisha na biashara za
magendo badala yake wawe ndio walinzi wa kuwafichua wahusika ili
kukomesha vitendo hivyo.
Mark
aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wafanyabiashara eneo la Horohoro
wilayani Mkinga ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani
Tanga ikiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa wao kulipa kodi kwa hiari.
Alisema
kutokana na wilaya hiyo kuwa mpakani mwa nchi ya Kenya hivyo ikiwemo
ukanda wa bahari na nchi kavu hivyo upo uwezekano wa vitendo vya namna
hivyo kufanya huku akiwataka viongozi hao kuvikemea na kutokuviruhusu
kwenye maeneo yao.
“Ndugu
zangu wevyeviti wa vijiji na vitongoji acheni kushirikia kwenye vitendo
vya biashara za magendo kwani kufanya hivyo tunaikosesha serikali
mapato yake ambayo yangesaidia kuchochea shughuli za kimaendeleo lakini
pia niwaambie kwamba tutakaobaini tutashughulikiwa kwa mujibu wa
sheria”Alisema Mkuu huyo wa wilaya
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kwamba wataendelea kushirikiana na TRA kufanya
operesheni za kupambana na vitendo vya biashara haramu za magendo ili
kuvikomesha kabisa kwani kutoka Tanga mpaka mpakani eneo la Horohoro
wana kilomita 70 za maji hivyo kupambana na hilo wataanzisha bandari
ndogo eneo la moa wilayani Mkinga.
Alisema
kwamba wanaanzisha ili kuiwezesha serikali kupata kodi huku akieleza
wanatarajia kulifanya hilo miezi michache ijayo watakuwa wamekwisha
kufungua huku akiwataka wafanyabiashara hao kutumia njia halali za
kupisha bidhaa zao badala ya zile za panya.
,dc
akizungumzia mashine za EFD alisema zinawasaidia wafanyabiashara
kutokana na kwamba zinaweka mahesabu yao vizuri kutokana na kwamba kila
kinachouxwa kinaonekana.hata hivyo aliwataka wafanyabiashara kutangaza
biashara zao ili ziweze kutambulika na hatimaye kuweza kupata wateja na
hatimaye kuwza kuingiza kipato.ulipaji wa kodi
Awali
akizungumza Afisa Elimu Mlipa Kodi wa TRA mkoani Tanga Salim Bakar
alisema kwamba hivi sasa walipa kodi wanatambua umuhimu wa kulipa kodi
kutokana na Serikali ya awamu ya tano kutekeleza mambo kwa vitendo na
kuonekana maendeleo mbalimbali ikiwemo madawa, elimu bure na miradi
mbalimbali inatekelezwa kupitia kodi hizo.
Naye
kwa upande wake ,Diwani wa Kata ya Duga (CCM) Ally Ally amesema umuhimu
wa kulipa kodi kwa wananchi ni mkubwa kutokana na kwamba maendeleo
yanayopatikana yanatokana na uwepo wa ulipaji wa kodi hizo.
“Mimi
kama diwani wa Kata ya Duga nitaendelea kuhakikisha ninahamasisha
wananchi kuendelea kulipa kodi kwa lengo la kusaidia kuchochea kasi ya
ukuaji wa maendeleo “Alisema
Hata
hivyo pia Afisa Habari wa Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoani Tanga (JWT)
Selestine Kiria aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi kwa
hiari ili kuwasaidia ukuaji wa maendeleo.
“Kwani
wafanyabiashara kulipa kodi ndio Taifa linaendelea lakini pia kuchochea
ukuaji wa maendeleo lakini pia hakikisheni mnatoa risiti wakati
mnapouza bidhaa zenu “Alisema
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇