Rais Dkt. John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Abiria wa Daladala iliyokuwa ikitoka Bukoba mjini kuelekea Karagwe mjini mara baada ya kuwasalimu wakati waliposimama katika Kituo cha Daladala kilichopo katika kijiji cha Kihanga nje kidogo ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Dkt. Magufuli akiwa amembeba mototo wa mmoja wa abiria wa daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Bukoba mjini kuelekea Karagwe mjini mara baada ya kuwasalimu wakati waliposimama katika Kituo hicho cha Daladala kilichopo katika kijiji cha Kihanga nje kidogo ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Dkt. Magufuli akizungumza jambo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondary Karagwe ambaye alikuwa akisafiri na daladala hiyo.PICHA NA IKULU |
Taarifa iliyotolewa jana Jumatano Julai 10, 2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema Rais Magufuli ameyasema hayo Kijijii cha Kihanga, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera alipokutana na abiria na dereva wa basi dogo linalofanya safari zake kati ya kati ya Bukoba na Karagwe.
Rais Magufuli amesema ajali nyingi za barabarani husababishwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu za usalama barabarani na kwamba jukumu la kuhakikisha sheria na taratibu hizo zinatekelezwa upo kwa watumiaji wote wa barabara hasa madereva wanaoendesha vyombo vya usafiri.
“Poleni na safari ndugu zangu, nimefurahi kuwaona na kuwasalimu, na wewe dereva hongera kwa kazi, fanya kazi zako kwa kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani, pia kumbuka kusali kabla na baada ya safari” alisema Rais Magufuli
Pia, Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwaeleza abiria ambao ni wanafunzi kusoma kwa juhudi masomo yao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇