Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Rais wa Senegal wamesisitiza kustawishwa uhusiano wa pande mbili katika nyanja zote.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif na Rais Macky Sall wa Senegal walitoa sisitizo hilo katika mazungumzo yao waliyofanya jana mjini Dakar, ambapo walijadili na kubadilishana mawazo kuhusu masuala muhimu zaidi ya pande mbili na matukio ya hivi karibuni ya kieneo na kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezungumzia safari yake hiyo nchini Senegal katika ukurasa wa Twitter pia kwa kuandika: Baada ya kuhudhuria mkutano Umoja wa Mataifa na kutembelea bara la Amerika, katika kituo cha nne cha safari yangu huko Dakar mji mkuu wa Senegal, yamefanyika mazungumzo muhimu baina ya pande mbili na Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Spika wa Bunge la nchi hiyo.
Dakta Zarif amesisitiza kwa kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakupa thamani kubwa kustawisha uhusiano na nchi za Afrika.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akiongoza ujumbe maalumu, jana aliwasili mji mkuu wa Senegal, Dakar akitokea Santa Cruz, Bolivia.../
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇