LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 19, 2019

MAREKANI YAKIRI KUSHIKILIWA KWA MTANGAZAJI WA PRESS TV

Mahakama moja ya Washington nchini Marekani imethibitisha kuwa mtangazaji wa televisheni ya Iran ya Press TV, Bi Marzieh Hashemi amewekwa kizuizini bila ya kosa lolote na kwa anwani ya "shahidi muhimu" katika kesi ambayo haikutajwa.
Nyaraka za mahakama hiyo ya Washington zilizotolewa na Jaji Beryl Howell, zinaonesha muwa Bi Marzieh Hashemi hajafanya kosa lolote. 
Maafisa wa Marekani wametangaza kuwa, mtangazaji Hashemi ambaye hadi sasa amefikishwa mahakamani mara mbili kwa ajili ya kutoa ushahidi, ataachiwa huru baada ya kukamisha kutoa ushuhuda wake. Hata hivyo maafisa hao hawakuainisha wakati wa kuachiwa huru mtangazaji huyo wa televisheni ya Press yenye makao yake makuu mjini Tehran. 
Kwa mujibu wa sheria ya zamani ya Marekani, Serikali ya Federali ya nchi hiyo inaweza kuwatia nguvuni watu bila ya tuhuma yoyote na kwa anwani ya "shahidi muhimu" wa faili au kesi. 
Mwandishi huyo wa habari na mtangazaji wa kanali ya televisheni ya Press TV ni mzaliwa wa Marekani na anaishi nchini Iran kwa miaka kadhaa sasa. Bi Marzieh Hashemi alikuwa safarini Marekani kumtembelea kaka yake ambaye ni mgonjwa pamoja na jamaa wengine wa familia yake.
Bi Hashemi alikamatwa siku ya Jumapili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa St. Louis Lambent, Missouri na kuwekwa kizuizini na Polisi ya Upelelezi ya nchi hiyo FBI. 
Marzieh Hashemi
Katika mawasiliano pekee aliyoweza kufanya na binti yake, Marzieh Hashemi ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika, aliyekuwa akiitwa Melanie Franklin na baadaye akasilimu baada ya kudhihirikiwa na nuru ya uongofu ya Uislamu, amesema, baada ya kukamatwa, alifungwa pingu na minyororo na kutendewa kama mhalifu.
Amesimulia pia kuwa, alivuliwa vazi la hijabu kwa nguvu na kupigwa picha bila ya mtandio wa kichwa baada ya kufikishwa mahabusu.
Maafisa wa Marekani wamemruhusu mtangazaji huyo wa televisheni kuvaa fulana tu na kumfanya alazimike kutumia fulana nyingine kujisitiri kichwa chake.
Maafisa wa jela ya Marekani wamemnyima pia Marzieh Hashemi haki ya kutumia chakula halali au cha walaji mbogamboga na kumpatia nyama ya nguruwe, ambayo imeharamishwa katika Uislamu. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages