LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2019

AYATULLAH MOVAHEDI-KERMANI: MAPAMBANO DHIDI YA UTAKATISHAJI FEDHA NA UGAIDI NI UONGO MKUBWA WA WAMAGHARIBI

  • Ayatullah Mohammad Ali Movahedi-Kermani
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran, Ayatullah Mohammad Ali Movahedi-Kermani amesema kwamba, lengo la kuundwa kundi eti la kumbana na utakatishaji wa fedha chafu la Financial Action Task Force (FATF) ni kufuatilia vyanzo vya fedha vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyingine.
Ayatullah Mohammad Ali Movahedi-Kermani ameyasema hayo katika hotuba ya Swala ya Ijumaa ya Tehran na kuongeza kuwa, madai ya nchi za Magharibi ya kupambana na utakatishaji fedha na ugaidi ni uongo mkubwa. Amesema kuwa, makao makuu ya utakatishaji fedha na kufadhili  ugaidi ni Marekani na Magharibi na kwamba nchi hizo kwa kushirikiana na utawala haramu wa Israel ndio waungaji mkono wakubwa wa ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kwa ujumla. 
Khatibu wa muda wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa, ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio iliyopambana na kuwafurusha kutoka Syria na Iraq wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) ambalo liliundwa na Marekani na washirika wake. Akiashiria jinsi viongozi wa Marekani walivyokiri kwamba walihusika katika kuanzisha kundi hilo la kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati kwa lengo la kuzigawa nchi za eneo hili, amesema kuwa, Marekani, utawala haramu wa Israel na vibaraka wao katika eneo hili ndio wafadhili wakubwa wa jinai dhidi ya raia madhlumu wa Yemen na wamefanya mauaji ya maelfu ya watoto na wanawake wasio na hatia wa nchi hiyo.
Mfumo wa FATF unaotumiwa na Wamagharibi kuikandamiza Iran ya Kiislamu na nchi nyingine
Kadhalika Ayatullah Movahedi-Kermani ameashiria jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina na kusema kwamba, baada ya hatua hasi za Rais Donald Trumo wa Marekani dhidi ya Wapalestina, wakazi wa eneo la Ukanda wa Gaza walianzisha maandamano ya amani ya Haki ya Kurejea katika kila siku ya Ijumaa ambapo askari wa utawala khabithi wa Israel wamekuwa wakifanya jinai na mashambulizi dhidi ya raia hao wasio na ulinzi na kuua mamia na maelfu ya wengine kujeruhiwa. 
Khatibu wa Muda wa Swala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amekosoa kimya cha nchi za Magharibi na Marekani ambazo ni waongo wakubwa kwa kujinadi kuwa watetezi wa haki za binaadamu na kwamba daima zimekuwa zikinyamazia kimya jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Israel na Saudia katika eneo la Mashariki ya Kati. Amesisitiza kwamba, njia pekee ya kukabiliana na utawala huo katili pamoja na Marekani ni muqawama na kusimama kidete na kwamba matokeo yake yanashuhudiwa huko Syria, Iraq, Lebanon, Palestina kwa kuondoka kwa fedheha Marekani kutoka Syria. Amesema kwamba kwa muda sasa wakazi wa Ukanda wa Gaza na Palestina wanapambana na dhulma na ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni na kwamba hakuna shaka kwamba hatimaye wataibuka washindi katika mapambano yao hayo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages