LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2019

CONGO DR YATAKA WITO WA AU WA KUCHELEWESHA TANGOZO LA MATOKEO YA MWISHO YA UCHAGUZI MKUU

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekataa wito wa Umoja wa Afrika (AU) wa kuchelewesha kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais, suala ambalo linazidisha shaka kuhusu matokeo ya uchaguzi huo.
Umoja wa Afrika ulitoa tangazo la ghafla jana Alkhamisi ukitaka kuchelewesha kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa sababu ya "shaka kubwa" kuhusu jinsi uchaguzi huo ulivyofanyika. Suala hilo linatia mashakani zoezi zima la uchaguzi wa rais wa Congo DR ambao ulitazamiwa kuwa wa kwanza utakaoshuhudia zoezi la kupokezana madaraka kwa njia ya kidemokrasia nchini humo katika kipindi chote cha miaka 59 ya uhuru wa Congo.
Wito huo wa Umoja wa Afrika unakuja siku kadhaa baada ya mgombea wa opinzani, Martin fayulu wa chama cha Lamuka kusisitiza kwamba matokeo ya uchaguzi huo yamechakachuliwa kwa faida ya Felix Tshisekedi aliyetangazwa kuwa mshindi wa kiti cha rais.
Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais wa Congo DR yalitazamiwa kutangazwa leo au kesho Jumamosi mara tuu Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo itakapotoa uamuzi kuhusu pingamizi zililotolewa na pande kadhaa likiwemo lile la mgombea wa chama cha Lamuka, Martin Fayulu.
Msemaji wa serikali ya Kinshasa, Lambert Mende amesema kuwa: "Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuiambia mahakama ya Congo ifanye nini, na wala hakuna nchi inayoweza kukubali mchakato wa mahakama zake udhibitiwe na taasisi ya kigeni."
Lambert Mende
Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imesema kuwa taasisi hiyo itatuma ujumbe huko Congo kuchunguza njia ya kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro uliojitokeza baada ya uchaguzi mkuu wa Disemba 31 mwaka uliomalizika.
Ujumbe huo utajumuisha Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika Moussa Faki na viongozi wengine kadhaa wa nchi za Afrika.  
Fayulu anasisitiza kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi huo kwa kupata zaidi ya asilimia 60 ya kura, lakini Tume ya Uchaguzi ilimtangaza mshindani wake, Felix Tshisekedi kuwa mshindi baada ya kufanya mapatano ya siri na kiongozi anayeondoka madarakani, Joseph Kabila. Serikali ya Kinshasa imekanusha madai hayo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages