Katibu Muhutasi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) mstaafu , Nyasigwa Heri (kushoto) alianza kwa kumshukuru Mungu kwa kumpa afya njema na kufikia muda wa kustaafu akiwa na nguvu na pia aliwashukuru makatibu muhtasi wote wa MUHAS kwa kuonyesha mfano.
Nyasigwa alisema "Hata wenzetu walio tanguli kustaafu nafikiri wakisikia hivi watasema sasa hivi tumebadilika kwa kuwa na ushirikiano wa kuwa na utamaduni wa kupongezana na kushirikiana katika shida na faraja,pia mzidi kumtegemea Mungu muda wote".
Aliongeza kwamba," Mzidishe upendo mahala pa kazi kuimarisha umoja huu na ushirikano kama mnao tuonyesha kwakutufanyia sherehe ambayo hapo nyuma hakukuwa na utaratibu huu".
Aliwaasa wanaobaki kazini kuwa Mungu ndiye muweza wa kila kitu na kumtanguliza Mungu watashinda na kutegua mitego ya kila aina, fitna, chuki,na udhaifu wa kila aina.
mzidi kutuombea, "alisema" wakati wa hafla yao ya kupongezwa baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheri ambapo alikuwa akifanya kazi katika Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi (MUHAS) Muhimbili. kulia ni Katibu Muhtasi mstaafu Janety Lutosha.
Katibu Muhtasi mstaafu, Janety Lutosha akizungumza jambo.
Makatibu Muhtasi wakiserebuka katika Ukumbi uliopo eneo la Chuo hicho
Makatibu Muhtasi wakiserebuka pamoja na wastaafu katika Ukumbi uliopo eneo la Chuo hicho
Katibu muhtasi, Elizabeth Boniface (kushoto) akiongoza sala kabla ya kufungua hafla hiyo jana katika ukumbi uliopo katika majengo mapya ya (MUHAS)
Katibu Muhtasi, Rehema Mamba ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya sherehe na mshehereshaji wa hafla ya kuwaaga makatibu muhtasi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) iliyofanyika Desemba 7, 2018.
Kwani tutakuwa tunapunguza msongo wa mawazo kwa kufurahi na kula pamoja, ile kamati yangu nafikiri mnajijua mtandike mkeka kwa ajili ya mwishoni mwa Desemba hii na hatutaki Januari tunataka Desemba tukijaaliwa tunakwenda kufurahi pamoja.
Lengo na madhumuni ni kufurahi kwa pamoja na kubadilishana mawazo na kujumuika kwa kucheza, kama mnavyojuwa sisi niwatu muhimu sana katika Taasisi zetu kwa hiyo tunatakiwa tuwe na furaha wakati wowote mahala pakazi na majumbani kwetu.
Baada ya kusema hayo nirudi kwa dada zangu wastaafu. Sisi tupo pamoja nanyi na hatutowafuta katika Group letu na pindi tutakapokuwa na jambo tutawajulisheni na halikadhalika nanyi mkiwa na jambo mtujulishe
Katibu Muhtasi wakisikiliza jambo wakati MC alipokuwa akizungumza jambo
Matibu Muhtasi wakigonganisha glasi yenye kinywaji cha shampeni kwa kutakiana afya njema na heri ya mwa mpya wa 2019
Severina Mnyaga akifungua shampeni wakati wa sherehe hiyo
Katibu Muhtasi, Neema Masima (kulia) amkimmiminia shampeni, Janeth Lutosha ambaye ni mmoja kati ya wataafu hao
Wataafu wakilishana kipande cha keki, kushoto ni Janeth Lutosha na Nyasigwa Heri
Margreth Lyimo (kulia) akimkabidhi bahasha Nyasigwa Heri yenye zawadi iliyotolewa na kamati ya maandalizi
Mwajabu Abdallh (kushoto) akimkabidhi Janeth Lutosha zawadi iliyotolewa na kamati ya maandalizi
Makatibu Muhtasi (MUHAS) katika picha ya pamoja na Wastaa walio kaa ambapo wawili hawajabahatika kufika (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).
Your Ad Spot
Dec 8, 2018
Home
Unlabelled
WASTAAFU BAADA YA MIAKA 40 KAZINI
WASTAAFU BAADA YA MIAKA 40 KAZINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇