Mufti Abubakari bin Zuberi akisoma dua na baadhi ya wajumbe kutoka taasisi ya Dhi Nureyn kwa ajili ya kuwaombea watoto waliolazwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati wa kambi maalum iliyofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na madaktari kutoka mradi wa Little Heart wa nchini Saud Arabia. Jumla ya watoto 70 na watu wazima wawili wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea ngao kutoka kwa Dkt. Jameel Alata ambaye ni mkuu wa msafara wa wataalamu wa afya kutoka mradi wa Little Heart wa nchini Saudi Arabia ambao wako katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ya siku saba kwa watoto wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nao.
Baadhi ya madaktari kutoka mradi wa Little Heart wa nchini Saudi Arabia ambao ni mradi wa afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao makuu yake mjini Londoni nchini Uingereza wakifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza madaktari hao baada ya kumalizika kwa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya kuzaliwa nayo iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) .
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tabu Nihuka akiwafungua watoto “cannula” ambao wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya kuzaliwa nayo iliyofanywa na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa mradi wa Little Heart wa nchini Saud ambao ni mradi wa afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao Makuu yake mjini Londoni nchini Uingereza. Jumla ya watoto 70 na watu wazima wawili wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua.
Picha na JKCI
Mufti Abubakari bin Zuberi akimkabidhi Katibu mkuu wa Taasisi ya Dhi Nureyn Shams Elmi Obsiye ngao ya kuipongeza Taasisi hiyo kutokana na kuwa kiunganishi kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mradi wa Little Heart wa nchini Saud Arabia ambao wamefanya kambi ya matibabu ya moyo na kutibu watoto 70 na watu wazima wawili wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo
Your Ad Spot
Dec 8, 2018
Home
Unlabelled
KUFUNGWA KWA KAMBI MAALUM YA MATIBABU KWA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO
KUFUNGWA KWA KAMBI MAALUM YA MATIBABU KWA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇