TAARIFA
Disemba 8, 2018Katika ufunguzi wa Semina ya Viongozi na watendaji wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Dar es salaam, Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi amesema CCM inaendelea na itaendelea kusimamia, kufuatilia na kushughulika na changamoto za wanawake muda wote.
Akieleza kwa undani dhamira hiyo Ndg. Polepole amesema lengo la CCM na Serikali yake ni kuinua wananchi na hususani wanawake, na kuwa CCM inasimamia na itasimamia masuala ya fedha za kuwezesha wanawake, maslahi ya wanawake kwenye masuala la huduma za afya na hivyo amewataka watendaji wa UWT kuendelea kuwasemea wanawake, kuwasikiliza wanawake na kuwatetea wanawake muda wote.
"Tunaomba UWT muendelee kuwa macho ya CCM, Masikio ya CCM katika maeneo yenu na muwasemee wanawake na mtakapotekeleza hili vizuri mtapata heshima kwa watanzania*_ amesema Ndg. Polepole
Aidha Ndg. Polepole ametumia mkutano huo kutoa angalizo na maelekezo kwa watendaji wa Serikali kufuatia tabia ya baadhi ya watendaji kutotambua kuwa miradi ya Serikali ni maekekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ikiwemo na mradi wa
DMDP (Dar es salaam Metropolitan Development Project).
*Upo Mradi wa kuendeleza Jiji la Dar es Salaam unaoitwa DMDP ambao unalenga kupunguza msongamano wa Magari Jijini Dar es Salaam, lakini Mradi huu umekuwa ukifafanuliwa kama mradi huru na bila kubainisha kwamba mradi huu ni maelekezo ya Ilani ya CCM Fungu la 39, kuanzia sasa husianisheni mradi huu na maelekezo ya Ilani ya CCM_* amesema Ndg. Polepole
Huu ni muendelezo wa Kazi za uimarishaji wa Jumuia za Chama, katika kuhakikisha ujenzi wa Chama Imara na Madhubuti.
Imetolewa na,
*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
*CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)*
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇